

Lugha Nyingine
Soko la utalii la Hainan lapata mwanzo mzuri wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Kwa mujibu wa takwimu za Idara ya Utalii, Utamaduni, Redio na Televisheni ya Mkoa wa Hainan, wakati wa Wiki ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, Hainan imepokea jumla ya watalii milioni 5.4113 na kupata jumla ya mapato yatokanayo na shughuli za utalii ya yuani bilioni 7.53, na kuleta mwanzo mzuri wa soko la utalii wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa Chuimilia wa China.
Kutokana na faida za sera endelevu za kutotozwa ushuru kwa bidhaa katika mkoa huo, manunuzi ya bidhaa zisizotozwa ushuru yamekuwa “kadi ya dhahabu ya biashara” ya Hainan. Wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China, maduka ya bidhaa zisizotozwa ushuru ya Hainan yalikuwa na ofa za aina mbalimbali za punguzo la bei ambazo zimekaribishwa na wanunuzi.
Mtalii anayetoka Mji wa Guiyang, Huang Ruijie alinunulia familia yake bidhaa zisizotozwa ushuru kwenye Duka lisilitozwa ushuru lililoko kwenye jengo la Riyue la Haikou. Alisema kuwa kununua bidhaa zisizotozwa ushuru kumekuwa ratiba muhimu ya kusafiri kwenda Hainan, pia wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China, kuna ofa nyingi za punguzo kubwa la bei, na ni nafuu sana kununua bidhaa zisizotozwa ushuru.
Wakati watalii wanaotoka nje ya Hainan wakifurahia kununua bidhaa zisizotozwa ushuru, watalii wengi kwenye kisiwa hicho wanapenda safari za utalii kwenye mazingira asili katika vijiji vilivyoko eneo la milima ya katikati ya Hainan. Chini ya Mlima wa Bawangling katika wilaya inayojiendesha ya Changjiang ya kabila la Wali, Wang Yiqin, mmiliki wa hoteli ya Mumian anaonekana kuwa na pilikapilika . Aliwaambia waandishi wa habari kuwa, sasa watu wengi zaidi wa mijini wanapenda vivutio vijijini, hasa katika majira ambapo maua ya Bombax ceiba yanachanua kikamilifu. Watu wengi hutumia fursa ya likizo kuleta watoto na wazee wao kufurahia likizo. “Naamini mustakabali wa shughuli za utalii vijijini zitaendelea vizuri zaidi .”
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma