“Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing inaleta maendeleo na ustawi”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 09, 2022

Picha iliyopigwa Februari 9, 2022 ikionesha wanamichezo wakifanya mazoezi kabla ya fainali ya mbio fupi ya mita 1,500 kwa wanaume ya kuteleza kwa kasi kwenye barafu katika Jumba la michezo la Mji Mkuu, mjini Beijing, China. (Xinhua/Xu Zijian)

BRUSSELS – Chombo cha habari cha mtandaoni mjini Brussels, Ubelgiji kimetoa maoni kwamba, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ni tukio muhimu la kuleta maendeleo na ustawi.

“China siku zote inashikilia wazo la kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi iliyo rafiki kwa mazingira, jumuishi, ya wazi na safi, ambayo linaendana na mageuzi ya michezo ya Olimpiki” inasema makala kwenye chombo hicho cha habari yenye kichwa "Michezo ya Majira ya baridi ya Beijing kuandika sura mpya ya Amani, maendeleo".

"Michezo ya Majira ya baridi ya Beijing ni ya kwanza katika historia kuwezesha sehemu zake zote za mashindano kutumia umeme unaozalishwa kwa nishati safi, ya kwanza katika historia kutumia kwa kiasi kikubwa teknolojia ya kaboni dioksidi katika kutengeneza barafu bila kutoa hewa ya kaboni, na ya kwanza katika historia kwa kutekeleza kikamilifu sera za maendeleo endelevu za IOC katika nyanja za uchumi, mazingira na jamii," inasema Makala hiyo.

Imeongeza kwamba, falsafa mpya ya maendeleo yenye uvumbuzi, uratibu, kijani, uwazi na maendeleo ya pamoja iliyooneshwa kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing italeta msukumo mkubwa katika maendeleo endelevu ya Dunia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha