Kwaya ya Watoto kutoka Milimani yashangaza Dunia katika Sherehe za Ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 11, 2022

Kwaya ya watoto wakiimba wimbo wa Olimpiki wakati wa sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing kwenye Uwanja wa Michezo wa Taifa hapa Beijing, Februari 4, 2022. (Xinhua/Cao Can)

Katika usiku wa Februari 4, kwaya ya watoto 44 kutoka kaunti yenye milima mingi ya Kaskazini mwa China iliimba wimbo rasmi wa Olimpiki katika sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022, wakivuta hisia za Dunia nzima kwa kujiamini katika macho yao na utulivu ya sauti zao.

“Tambarare, milima, na bahari vinang'aa pamoja nawe, kama hekalu kubwa lenye rangi nyeupe na zambarau......” watoto hao waliimba kwa lugha ya Kigiriki.

Maneno ya wimbo huo yanafaa watoto hao, kwa kuwa wanatoka eneo la milima.

Kutafuta “Manukato ya Dunia”

Tokea Michezo ya Olimpiki ya kwanza ya Mwaka 1896, wimbo wa Olimpiki huimbwa kwenye sherehe za ufunguzi katika karibu kila toleo la Michezo ya Olimpiki.

Timu ya maandalizi ya sherehe za ufunguzi na ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022 ilifanyia usaili wa waombaji wengi, lakini wote walishindwa kukidhi vigezo. Kisha timu hiyo iliona video ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Malan ya Kijiji cha Fuping wakiimba nyimbo.

“Wenye kupendeza, wasafi na wenye haya,” huu ndiyo mtazamo wa kwanza wa Ma Xiaojing, mfanyakazi wa timu hiyo kuhusu watoto hao. “Unaweza kujua baadhi yao wana udadisi na kutaka kuongeana nawe. Lakini wanaona haya sana na kujificha nyuma ya walimu wao,” alisema Ma.

Ma na wenzake walitembelea shule kadhaa na kufanikiwa kukusanya kundi la watoto. Waliporudi Beijing, timu hiyo ya kuandaa sherehe ilisikia sauti za watoto kwa mara ya kwanza kwa kupitia video. Sauti zao zilikuwa kubwa na nyororo, ingawa siyo toni zote ni sahihi.

Walipomaliza kuimba, kiongozi mkuu Zhang Yimou alivunja ukimya kwa kupiga makofi.

“Hii ndiyo sahihi. Sauti hiyo ya malaika ya watoto hao ndiyo niliyotafuta – manukato ya Dunia,” alisema Zhang.

Nyimbo za Milima

Mnamo 2003, Deng Xiaolan, ambaye Baba yake Deng Tuo aliwahi kuendesha kijijini Malan gazeti la Jinchaji lililojulikana sana, alianza kujitahidi kuwasaidia wanakijiji huko ambao walikuwa wamemlea hadi alipofikisha umri wa miaka 3. Hii ilileta kuasisiwa kwa bendi ya Malan, ambayo baadaye imebadilika kuwa Kwaya ya Maua ya Malan.

Muziki ulileta uhai zaidi kwa kijiji hicho kidogo na kuwawezesha kusikika, lakini hakuwa na mtu yeyote aliyetarajia watoto hao wataweza kusikika kwenye jukwaa kubwa namna hiyo la Olimpiki.

Katika miezi minne kabla ya sherehe za ufunguzi, watoto hao 44 walimaliza kazi ngumu sana – kujifunza kuimba wimbo kwa lugha ya Kigiriki, na kufanya hivyo bila ya ala za muziki.

Kila siku, wimbo huo wa Olimpiki unasikika mjini kote, ukisafiri kwenye milima na tambarare mpaka Beijing.

Na katika asubuhi moja mapema ya Januari 2022, watoto walipanda basi ya kwenda Mji Mkuu wa China, safari ya saa zipatazo tano.

Kutoka Milimani mpaka Duniani

Hata wavulana watundu zaidi wa kwaya hiyo walishangaa sana walipoingia uwanja mkubwa wa “Kiota cha Ndege”.

Li Zhengze, ambaye alizaliwa 2010, alifikiria safari yake ya kwenda Beijing kwa mara nyingi. Alikumbuka namna alivyoingia ndani ya uwanja huo. “Ni tofauti na nilivyouona kwenye video, unawezaje kuwa ni mkubwa namna hiyo?”

Alikwepo pia Liang Youlin, ambaye mama yake alijaribu kumsomesha kaligrafi ya Kichina na sanaa ili kumfanya awe mtulivu lakini alishindwa. Sauti yake ilikuwa inatetemeka wakati wa mazoezi kwa mara ya kwanza.

Kusema kweli, hii ilikuwa changamoto kwa watoto hao, ambao waondoka nyumbani wakati wa mwaka mpya wa jadi wa China na kusafiri peke yao kwa mara ya kwanza. Kutekeleza hatua za kujikinga dhidi ya UVIKO-19 na mpango wa mazoezi pia si rahisi kwa watoto hao wanaopenda kucheza na kuwa na udadisi wa nje ya milima.

Lakini wana njia zao za kutatua changamoto hizo. “Wakati wa kusimama jukwaani, tunafikiria hadhira kuwa miti ya milimani, au nyota za angani,” mmojawapo wa watoto hao alisema.

Tarehe 4, Februari, watoto hao waliimba wimbo rasmi wa Olimpiki kwa sauti safi na nzuri. Chini ya mwanga wa taa, walileta furaha na fikra bora kwa Dunia kwa njia ya kujiamini, kama kiongozi Zhang alivyotazamia. 

Watoto wakifanya mazoezi ya sherehe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha