Timu ya China yaweka rekodi bora linganifu kwa medali za dhahabu ilizopata kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 15, 2022

Xu Mengtao mwenye umri wa miaka 31 ambaye ameshiriki kwa mara nne kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi hatimaye ametimiza ndoto yake hapa Beijing. Ametwaa medali ya dhahabu kwa mchezo wa kuteleza kwa ustadi kwa mtindo huru kwenye theluji kwa wanawake. Hii ni medali ya dhahabu ya tano ambayo China imepata kwenye Michezo hiyo ya Olimpiki na imeweka rekodi bora zaidi ya idadi ya medali za dhahabu ambazo Timu ya China imewahi kupata kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi.

Mchezaji wa Timu ya China Xu Mengtao akifurahia ushindi baada ya mchezo wa kuteleza kwa ustadi kwenye theluji na kuruka hewani kwa wanawake Februari 14 (Xinhua/Mpiga picha: Xiao Yijiu)

Utelezaji wa Xu Mengtao kwenye theluji umekuwa mzuri sana. Kuanzia hatua ya mashindano ya kufuzu nafasi ya kushiriki hadi fainali, alipata zaidi ya alama 100 katika kila mruko. Hatimaye Xu Mengtao ametimiza ndoto yake. Hii ni mara ya kwanza kwa mchezaji wa kike wa Timu ya China kutwaa ubingwa kwenye mchezo huo katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi. Pia ni medali ya dhahabu ya tano kwenye michezo ya mwaka huu ambayo imeweka rekodi bora zaidi ya kulingana na idadi ya medali za dhahabu ambazo Timu ya China ilipata kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Vancouver Mwaka 2010.

Mchezaji wa Timu ya China Xu Mengtao akishiriki kwenye fainali ya mchezo wa kuteleza kwa ustadi kwenye theluji na kuruka hewani kwa wanawake Februari 14. (Xinhua/Mpiga picha: Xiao Yijiu)

Mchezaji wa Timu ya China Su Yiming akishiriki kwenye mashindano ya kupata nafasi ya kufuzu fainali ya mchezo wa kuteleza kwa kasi kwenye theluji kwa kuruka angani kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing Februari 14. (Xinhua/Mpiga picha: Li Ziheng)

Wachezaji wa Timu ya China Wang Shiyue (Kushoto) na Liu Xinyu wakishiriki kwenye mashindano ya mchezo wa kuteleza kwenye barafu na kucheza dansi kwa mtindo huru kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing Februari 14. (Xinhua/Mpiga picha:Cao Can)

Mashindano ya mchezo wa kuteleza kwa kasi kwenye barafu kwa kutumia kigari kwa mtu mmoja ambao ni mpya katika michezo ya mwaka huu, yamemalizika Februari 14. Wachezaji wa Timu ya China Huai Mingming na Ying Qing walipata nafasi ya sita na ya tisa, na mchezaji wa Timu ya Marekani Kaillie Humphries alitwaa ubingwa.

Wachezaji Wang Shiyue na Liu Xinyu walipata mafanikio mazuri ya Timu ya China katika mchezo wa kuteleza kwenye barafu na kucheza dansi. Ikiwa ni timu pekee ya Bara la Asia kwenye fainali, wachezaji hawa wawili hatimaye walipata nafasi ya 12. Wachezaji Gabriella Papadakis na Guillaume Cizeron wa Timu ya Ufaransa walitwaa ubingwa wa mchezo huo.  

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha