Eneo la Kitanzi la kudhibiti UVIKO-19 kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing ni thabiti: The Independent

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 15, 2022

Wanamichezo wakishiriki katika mazoezi kabla ya raundi ya 8 ya mchezo wa Curling kwa Wanawake kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 kati ya Japani na Korea Kusini katika Kituo cha Taifa cha Kuogelea huko Beijing, Mji Mkuu wa China, Februari 14, 2022. (Xinhua/Huang Xiaobang)

LONDON, Februari 14 (Xinhua) – Gazeti la Uingereza la The Independent limesema kwamba, kuleta zaidi ya watu 15,000 kutoka pembe zote za Dunia hadi Beijing kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi kunaleta hatari kubwa ya kuenea UVIKO-19 nchini China. Hata hivyo, mfumo wa kutenga eneo la kitanzi kuepuka maambukizi ya virusi vya korona umethibitishwa kuwa thabiti.

Habari kutoka Gazeti hilo Ijumaa ya wiki iliyopita zinasema kwamba, wiki moja tangu michezo hiyo ianze, huku kukiwa na eneo la kitanzi ambalo linaruhusu washiriki kutokwenda karantini lakini linazuia shughuli zao ili kuepuka kukutana na idadi kubwa ya watu nje ya eneo hilo, kumekuwa na maambukizi 490 yaliyothibitishwa ya virusi vya korona- na sehemu kubwa ya maambukizi hayo ni yasiyo na dalili za UVIKO-19 na hakuna ripoti za maambukizi kutoka nje ya eneo la kitanzi.

Gazeti hilo limeongeza kwamba, nje ya eneo la kitanzi la Olimpiki, maisha yanaendelea kama kawaida kwa watu wengi katika mji mkuu wa nchi hiyo. Na kusema kuwa watu wamekuwa wakifuatilia Michezo hiyo kwenye simu za kisasa au TV.

Kwa mujibu wa makala hiyo, mbinu ya China katika kudhibiti maambukizi ya UVIKO-19 imezuia virusi hivyo vya korona, huku vifo 4,636 vikiripotiwa tangu kuanza kwa janga hilo, ikiwa ni sehemu ndogo ya vifo vilivyoripotiwa hadi sasa katika mataifa mengine makubwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha