“Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing inaonesha uthabiti wa michezo katikati ya janga la UVIKO”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 15, 2022

DUBAI – Vyombo mbalimbali vya habari vya Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu vimeripoti kwamba, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing inayoendelea mjini Beijing, nchini China imethibitisha kwa Dunia utahimilivu wa michezo katikati ya janga la UVIKO-19.

Licha ya changamoto kubwa chini ya hali ya sasa, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing imepata "mwanzo mzuri pamoja na hatua zote zilizowekwa ili kuhakikisha usalama wa wale wanaoshiriki," inasema tahariri ya Gulf News, gazeti la kila siku la Kiingereza huko Dubai.

Mwanamfalme wa Abu Dhabi wa UAE Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan "alisifu sherehe za ufunguzi na mpangilio wa hali ya juu wa Michezo," Shirika la Habari la Emirates limesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Mwanamfalme huyo aliyealikwa kuhudhuria sherehe za ufunguzi na kukutana na Rais Xi Jinping wa China kando ya Michezo hiyo, pia "aliitakia mafanikio mema katika kuimarisha madaraja ya uelewano na urafiki kati ya vijana duniani, hivyo kuimarisha misingi ya amani na kuishi kwa pamoja katika jukwaa la kimataifa," imesema taarifa hiyo.

"Uwezo wa Serikali ya China kuandaa shughuli kubwa ya kimataifa wakati wa janga hili ni wa kupongezwa sana," Liza Grey, mtaalamu wa mawasiliano kutoka Dubai amesema.

"Inaeleza vema kuhusu kauli mbiu ya Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu –Pamoja kwa Mustakabali wa pamoja wa baadaye - kwamba sote tunaweza kuondokana na janga hili ikiwa tutaonesha mshikamano, na michezo imethibitisha hilo," ameongeza.

Kwa kuzingatia kuheshimiana na kushirikiana, uhusiano kati ya UAE na China "umeingia katika zama mpya na maalum," inasema makala iliyochapishwa kwenye gazeti la Kiingereza la The National, la Abu Dhabi ikimnukuu Balozi wa UAE nchini China Ali Obaid Al Dhaheri.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha