Makala ya Rais Xi Jinping kuhusu utawala wa sheria wa Ujamaa wenye umaalumu wa China yachapishwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 16, 2022

BEIJING - Makala ya Rais Xi Jinping kuhusu kufuata njia ya utawala wa sheria wa Ujamaa wenye umaalumu wa China na kuendeleza mfumo wa utawala wa sheria wa Ujamaa wenye umaalumu wa China imechapishwa.

Makala ya Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, imechapishwa Jumatano (leo) katika toleo la nne la mwaka huu la Jarida la Qiushi, Jarida Kuu la Kamati Kuu ya CPC.

Makala hiyo inasema, kwa vile China sasa iko katika hatua muhimu ya kufikia ustawi mkubwa wa taifa, ni muhimu kutekeleza vyema jukumu la utawala wa sheria katika kuimarisha msingi, kukidhi matarajio na kudumisha maendeleo ya muda mrefu.

Inasisitiza kuzingatia mwelekeo sahihi katika kujenga mfumo wa utawala wa sheria, na kudumisha asili yake ya ujamaa wenye umaalumu wa China. Makala pia inatoa wito wa kuwa makini na thabiti katika masuala makubwa kama vile kushikilia uongozi wa jumla wa CPC na kuhakikisha wananchi ndiyo waendeshaji wa nchi, na kujilinda dhidi ya kupotoshwa na fikra mbovu za Magharibi.

Makala hiyo inahimiza kuharakisha kazi ya kutunga sheria katika baadhi ya sekta muhimu, ikitaja nyanja kama vile usalama wa taifa na uchumi wa kidijitali.

Kuhusu kuimarisha mageuzi katika utawala wa sheria, makala hiyo inaangazia kanuni na msingi, na kusisitiza kwamba mageuzi katika utawala wa sheria hayatauchukulia mfumo au utendaji wa nchi za Magharibi kama "kigezo."

Makala hiyo pia inatoa wito wa kuboreshwa zaidi kwa sheria zinazohusu mambo ya kigeni na kanuni za kukabiliana na vikwazo kutoka nchi za Magharibi, kuingiliwa mambo ya ndani na "mamlaka ya mkono mrefu," pamoja na kuimarishwa kwa utafiti na uenezi wa nadharia juu ya utawala wa sheria.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha