

Lugha Nyingine
Eneo la Biashara Huria la Afrika linaendelea kwa hatua madhubuti, Ushirikiano wa China na Afrika wapata fursa mpya
Picha iliyopigwa Februari 14 ikionesha bandari kubwa zaidi nchini Ghana, Bandari ya Tema. (Xu Zheng/Xinhua)
Tangu kuanzishwa Januari, 2021, ujenzi wa Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (AfCFTA) umekuwa ukiendelea kwa hatua madhubuti na kusukuma mbele mtandao wa uchumi wa Bara la Afrika wakati linapokabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo janga la UVIKO-19. Wadau wanasema, fursa mpya za ushirikiano wa Afrika na China zinazotokana na eneo hilo la biashara huria zinaanza kutokea hatua kwa hatua.
Katibu Mkuu wa AfCFTA Wamkele Mene alipohojiwa na vyombo vya habari vya Afrika mwezi uliopita alisema, hivi sasa zaidi ya nchi 39 zimeripoti kwa Umoja wa Afrika (AU) kwamba zimeidhinisha makubaliano kuhusu Eneo la Biashara huria la Bara la Afrika. Nchi wanachama wa AU zimefikia makubaliano juu ya ushuru forodha wa zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa zilizozalishwa barani Afrika, na zimeanzisha mfumo wa kutatua migongano.
Januari 13, mwaka huu, sektretarieti ya AfCFTA pamoja na Benki ya Uagizaji na Uuzaji wa bidhaa ya Afrika (Afreximbank) na mashirika mengine yalizindua rasmi mfumo wa malipo na mahesabu wa kidigitali wa Afrika huko Accra, mji mkuu wa Ghana, ambao umeziwezesha nchi za Afrika kutumia fedha zao kulipa kwa kasi na salama katika bara hilo. Inakadiriwa mfumo huo utaokoa gharama ya malipo ya Dola za Marekani bilioni 5 kwa Afrika.
Mene alisema, hatua hizo zimeonesha mwelekeo wa kusonga mbele kwa eneo la biashara huria la Afrika, na pia umeonesha nia ya nchi za Afrika ya kuhimiza kuunganisha soko la ukanda huo, na hali hiyo itahimiza zaidi biashara na uwekezaji katika Bara la Afrika na kuharakisha mchakato wa mtandao wa viwanda.
Takwimu za Idara Kuu ya Forodha ya China zinaonesha, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na Afrika Mwaka 2021 ilizidi Dola za Marekani bilioni 250, ambayo iliweka rekodi mpya tokea 2014.
Tovuti ya Wizara ya Biashara ya China ilitoa habari Novemba, 2021 ikisema, Wizara hiyo na sekretarieti ya AfCFTA zimesaini kumbukumbu za maelewano kuhusu kuanzishwa kwa kikundi cha wataalam wa ushirikiano wa kiuchumi. Naibu Waziri wa Biashara wa China Qian Keming alisema, ujenzi wa AfCFTA pamoja na kuhimiza ustawi wa Afrika, pia utaleta fursa muhimu kwa maendeleo ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika.
Picha iliyopigwa Februari 14 ikionesha bandari kubwa zaidi nchini Ghana, Bandari ya Tema. (Xu Zheng/Xinhua)
Picha iliyopigwa Februari 14 ikionesha bandari kubwa zaidi nchini Ghana, Bandari ya Tema. (Xu Zheng/Xinhua)
Picha iliyopigwa Februari 14 ikionesha bandari kubwa zaidi nchini Ghana, Bandari ya Tema. (Xu Zheng/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma