China yashika kasi Kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022 huku ikiongeza medali za dhahabu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 17, 2022

Mwanamichezo wa timu ya China Qi Guangpi. (Picha/Xinhua)

BEIJING - China ilipanda hadi nafasi ya nne kwenye jedwali la orodha ya medali za Olimpiki ambazo nchi washiriki wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 zimeshinda baada ya mwanamichezo mkongwe wa kuteleza kwenye theluji na kuruka hewani kwa ubao Qi Guangpu kuipatia nchi mwenyeji wa michezo hiyo medani yake ya saba ya dhahabu Jumatano wiki hii.

Zikiwa zimesalia siku nne kabla ya Michezo hiyo kufungwa, China sasa ina medali saba za dhahabu, nne za fedha na mbili za shaba. Norway inaongoza kwa medali 13 za dhahabu, ikifuatiwa na Ujerumani yenye medali 10 za dhahabu na Marekani yenye 8 za dhahabu.

Katika fainaili hiyo ya kusisimua, washiriki watano kati ya sita waliofika fainali ya mchezo huo wa kuteleza kwenye theluji na kuruka hewani kwa ubao kwa wanaume walitumia ujuzi kwa ugumu wa digrii 5.000, lakini ni Qi pekee ndiye alitekeleza vyema na kufikisha alama 129.0 zilizompa ushindi na medali hiyo ya dhahabu.

Ni medali ya tatu ya michezo ya kuteleza kwenye theluji na kuruka hewani kwa China, kufuatia ushindi wa medali ya fedha katika mashindano hayo kwa jinsia mchanganyiko, na dhahabu katika mashindano ya aina hiyo kwa wanawake aliyoshinda Xu Mengtao.

“Hii ni Olimpiki yangu ya nne kushiriki, nimejifunza mengi, huu ni wakati muafaka kwangu wa kutwaa medali ya dhahabu nchini China, nchi yangu ya asili, nina furaha sana watu wangu wapo pamoja nami, naweza kuhisi wamefurahia sana." amesema Qi baada ya fainali.

Huku Michezo hiyo ikikaribia kumalizika, Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imesifu uzuiaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona katika Michezo hiyo, ambayo imeshuhudia idadi ya visa vipya vya kila siku vya UVIKO-19 vinavyoripotiwa ndani ya eneo la kitanzi la michezo hiyo ikipungua hadi sifuri mnamo Februari 13.

"Nadhani wakati mwingine tunasahau kuwa kweli tuko katikati ya janga la Dunia. Na tunaandaa moja ya mashindano magumu zaidi ya kimataifa au tukio kubwa la Dunia kwa mafanikio," msemaji wa IOC Mark Adams amesema.

Mwanamichezo wa timu ya China Qi Guangpi. (Picha/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha