

Lugha Nyingine
China yasikitishwa sana na ukandamizaji wa India dhidi ya kampuni za China na APPs
BEIJING - Wizara ya Biashara ya China imeonesha masikitiko makubwa juu ya ukandamizaji wa India dhidi ya kampuni za China na program za mtandaoni (APPs) zinazohusiana, ikisema tabia hiyo imevunja haki na maslahi halali ya kampuni za China.
"Tumegundua kuwa wawekezaji wa kigeni, ikiwa ni pamoja na kampuni za China, wanazidi kuwa na wasiwasi kuhusu mazingira ya uwekezaji nchini India," amesema Gao Feng, Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China (MOC), katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi wiki hii wakati akijibu maswali kuhusu marufuku ya APP za Kampuni za China yaliyotangazwa na Serikali ya India.
"Tunatumai India itaboresha mazingira yake ya kibiashara na kuwatendea kwa usawa, kwa uwazi na bila ubaguzi wawekezaji wote wa kigeni, pamoja na kampuni za China" amesema.
Akibainisha kuwa China na India ni wenzi muhimu wa kiuchumi, Gao amesema anatumai kuwa India itachukua hatua madhubuti kudumisha mwelekeo mzuri wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa pande hizo mbili.
Kwa mujibu wa Wizara ya Bishara ya China, Mwaka 2021 biashara kati ya nchi hizo mbili iliongezeka kwa asilimia 43 na kufikia dola za Kimarekani bilioni 125.7.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma