China yaongeza orodha ya kuagiza bidhaa za rejareja za biashara kwenye tovuti za mtandao

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 22, 2022

Mpeleka vifurushi wa Kampuni ya biashara ya e-commerce Express Sunny akipakia migizo huko Horgos, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, Kusini Magharibi mwa China Juni 3, 2021. (Xinhua/Gu Yu)

Wizara ya Fedha ya China imesema, kuanzia Machi 1, 2022, China itaendelea kuongeza orodha ya kuagiza bidhaa za rejareja za biashara kwenye tovuti za mtandao.

Wizara hiyo pamoja na wizara saba nyingine zimetoa taarifa ya pamoja inayosema kuwa, orodha hiyo kwa jumla itaongeza aina 29 za bidhaa, zikiwemo vifaa vya kuteleza kwenye theluji, juisi ya nyanya na vifaa vya mchezo wa golu.

Bidhaa zote zilizomo kwenye orodha hiyo zinahitajiwa sana na wateja wa China katika miaka ya hivi karibuni, alisema Gao Lingyun, mtafiti kutoka Taasisi ya Sayansi ya Kijamii ya China.

“Marekebisho hayo yataongeza ugavi wa bidhaa wa soko la ndani, kukidhi mahitaji ya wateja ya kutarajia kuishi maisha ya raha, na kutoa fursa nyingi zaidi kwa kampuni za nchi za nje,” alisema Gao.

Orodha hiyo ilitolewa Aprili 2016 na imekuwa ikiongezwa mara kadhaa, huku aina za bidhaa zake zikiongezeka, hali ambayo imesaidia kuhimiza maendeleo ya biashara ya kimataifa kwenye tovuti za mtandao na biashara bora, alisema Tian Gaofeng, Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Biashara katika Huduma la China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha