Timu ya China ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing yaundwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 22, 2022

Wachezaji wakihudhuria mkutano wa uhamasishaji wa Timu ya China ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing katika Kituo cha Usimamizi wa Michezo ya Walemavu cha China cha eneo la Shunyi, Beijing Februari 21. (Cai Yang/Xinhua)

Timu ya China ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing imeundwa hapa Beijing Februari 21.

Hii ni mara ya sita kwa China kupeleka timu kushiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi, na pia ndiyo timu kubwa zaidi, yenye wachezaji wengi zaidi, na kushiriki michezo mingi zaidi tangu ianze kushiriki kwenye michezo hiyo.

Idadi ya jumla ya watu katika timu hiyo ni 217, wakiwemo wachezaji 96, ambao wa kiume 68 na wa kike 28, na wengine 121 ni makocha, wafanyakazi, wasaidizi na madaktari na wauguzi.

Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing itafanyika kuanzia Tarehe 4 hadi 13, Machi, ambapo Timu ya China itashiriki kwenye mashindano ya michezo mikubwa sita na michezo midogo 73.

Wachezaji wakihudhuria mkutano wa uhamasishaji wa Timu ya China ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing katika Kituo cha Usimamizi wa Michezo ya Walemavu cha China cha eneo la Shunyi, Beijing Februari 21. (Cai Yang/Xinhua)

Wachezaji wa mchezo wa curling ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing wakipiga picha pamoja na makocha katika Kituo cha Usimamizi wa Michezo ya Walemavu ya China cha eneo la Shunyi, Beijing baada ya mkutano wa uhamasishaji wa Timu ya China ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing Februari 21. (Cai Yang/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha