

Lugha Nyingine
Bunge la Umma la China laanza kikao cha kamati ya kudumu
Li Zhanshu,Spika wa Bunge la Umma la China (NPC), akiongoza mkutano wa kwanza wa mashauriano wa Kikao cha 33 cha Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la 13 kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, Mji Mkuu wa China, Februari 27, 2022. (Xinhua/Zhang Ling)
BEIJING - Kamati ya Kudumu ya Bunge la 13 la Umma la China (NPC), imeanza mkutano wake wa 33 Februari 28 kujiandaa na mkutano ujao wa tano wa mwaka wa Bunge la Umma la 13, utakaofunguliwa Machi 5.
Li Zhanshu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya NPC, ameongoza mkutano wa kwanza wa kikao hicho. Jumla ya wajumbe 157 wa Kamati ya Kudumu ya NPC walihudhuria kikao hicho.
Wabunge walipitia ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya NPC. Ripoti hiyo ya kazi itawasilishwa kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma Mwezi Machi kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa.
Wajumbe hao pia walipitia rasimu ya ajenda ya kikao cha mwaka cha NPC, orodha ya rasimu ya majina ya kikundi cha wenyeviti wa mkutano na katibu mkuu wa mkutano huo wa mwaka, na orodha ya rasimu ya majina ya wajumbe waalikwa kuketi kwenye mkutano wa mwaka kama washiriki wasiopiga kura.
Walijadili rasimu ya uamuzi juu ya safu za askari walio kazini wa Jeshi la Ukombozi la Umma, rasimu ya uamuzi wa kuanzisha mahakama ya masuala ya fedha ya Chengdu-Chongqing, na ripoti ya utekelezaji wa uamuzi wa Kamati ya Kudumu ya NPC kuhusu utaratibu wa kusuluhisha kesi za hakimiliki za ubunifu.
Wajumbe hao wa bunge la umma pia walipitia ripoti kuhusu sifa za baadhi ya wajumbe, pamoja na miswada inayohusiana na watendaji.
Li pia aliongoza kikao cha Baraza la Wenyeviti wa Kamati ya Kudumu ya NPC baada ya kikao cha kwanza cha mashauriano.
Li Zhanshu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China (NPC), akiongoza mkutano wa 110 wa Baraza la Wenyeviti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la 13 kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, Februari 27, 2022. (Xinhua/Zhang Ling)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma