Utaratibu wa uratibu wa ngazi ya juu katika Michezo ya Paralimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing wazinduliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2022

Picha iliyopigwa Februari 10, 2022 ikionesha kileta bahati cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya walemavu ya Beijing 2022 Shuey Rhon Rhon aliyetengenezwa kwa karatasi huko Shenyang, Mji Mkuu wa Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China. (Xinhua/Yang Qing)

BEIJING - Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu (IPC) na Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 (BOCOG) zimefanya mkutano wao wa kwanza wa ngazi ya juu kwa njia ya video Jana Jumapili, ambapo walijadili maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya walemavu.

Rais wa BOCOG Cai Qi amesema, "Ubadilishaji wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya baridi ulianza tangu kufungwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing. Maeneo ya Michezo, huduma, utangazaji na mawimbi kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ijayo viko tayari, na vimetambuliwa na wataalamu wa IPC."

"Tuna imani ya kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya baridi kama ilivyokuwa kwa ile ya Olimpiki, na BOCOG itafanya kazi kwa karibu na IPC ili kutimiza lengo hilo," Cai ameongeza.

Rais wa IPC Andrew Parsons amepongeza maandalizi ya BOCOG kwa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya baridi, na kuongeza kuwa China imefanya juhudi kubwa kuwavutia zaidi watu wenye ulemavu kushiriki katika michezo ya msimu wa baridi.

"Huduma zinazotolewa na wafanyakazi wa kujitolea huko Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022 zilitufanya tuhisi ukarimu wa watu wa China," Parsons amesema.

"Sote tunatumai kuimarisha zaidi uratibu wetu na kuona wanamichezo kutoka kote Duniani wakifurahia michezo hiyo.”

Cai Qi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Walemavu ya Beijing 2022 (BOCOG), akihutubia wakati wa sherehe ya kufunga Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 kwenye Uwanja wa Michezo wa Taifa wa Beijing, Mji Mkuu wa China, Februari 20, 2022. (Xinhua/Li Ga)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha