Maofisa Viongozi wa CPC wawasilisha ripoti za kazi kwa Kamati Kuu ya CPC na Xi Jinping

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 01, 2022

BEIJING - Maofisa Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) hivi karibuni wamewasilisha ripoti kuhusu kazi zao kwa Kamati Kuu ya CPC na Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC.

Viongozi hao waliowasilisha ripoti ni wajumbe wa Ofisi ya Siasa na Sekretarieti ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na wajumbe wa vikundi vya uongozi wa Chama vya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, Baraza la Serikali la China na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China pamoja na makatibu wa vikundi vya uongozi wa Chama vya Mahakama Kuu ya Umma ya China na Idara kuu ya Uendeshaji wa Mashtaka ya China.

Baada ya kusoma ripoti zao za kazi, Xi amewataka wachukue hatua halisi za kihistoria kwa kukaribisha Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC utakaofanyika hivi karibuni.

Xi amewataka kudumisha umoja wa hali ya juu na Kamati Kuu ya CPC na kutekeleza kwa uthabiti sera na mipango yake ya kazi.

Xi amewataka kusukuma sekta na idara zilizo chini ya uangalizi wao kutekeleza kikamilifu, kwa usahihi na kwa kina mawazo mapya ya maendeleo na kuharakisha uundaji wa mfano mpya wa maendeleo ili kukuza maendeleo ya kiwango cha juu.

Pia amewataka watimize wajibu wa uongozi katika kazi ya Chama kijiendeshe kwa nidhamu kali.

Ripoti za maofisa viongozi hao zilifanya majumuisho ya uzoefu wao mwaka 2021 na kueleza mambo makuu ya kazi za baadaye, ambazo pamoja na mambo mengine zinalenga kuongoza katika kusoma na kutekeleza Mawazo ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye umaalum wa China kwa zama Mpya, na kufanya juhudi za kuenzi moyo wa Chama wa kuanzisha Jamhuri ya Watu wa China. Pia kuboresha mwenendo wa Chama na kung'oa kabisa ufisadi katika nyanja wanazozisimamia na kuwa mifano mizuri ya kufuata maadili na kujizuia kwa nidhamu, na kutii kwa hiari uangalizi wa utendaji wa kazi zao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha