Lugha Nyingine
Rais Xi asisitiza kukuza kampuni za China za kiwango cha kimataifa
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amehimiza juhudi za kuharakisha kukuza makampuni ya biashara ya China yenye kiwango cha kimataifa na kuimarisha ukuzaji wa vipaji katika taaluma za msingi.
Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, ameyasema hayo alipokuwa akiongoza mkutano wa 24 wa Kamati Kuu ya kuimarisha mageuzi.
Mkutano huo umepitia na kupitisha miongozo kadhaa kuhusu masuala yaliyotajwa hapo juu, pamoja na mapendekezo mengine ya kuendeleza maendeleo ya kiwango cha juu ya ujumuishaji wa kifedha na kuimarisha uwezo wa makampuni yanayomililkiwa na Serikali (SOEs) wa kuendeleza teknolojia halisi za China.
Xi ambaye pia ni Mkuu wa Kamati ya kuimarisha mageuzi amesema kuwa, China itaharakisha ujenzi wa kampuni za kiwango cha kimataifa zenye bidhaa na chapa bora, uvumbuzi unaoongoza, na usimamizi wa kisasa.
Xi amesema, China itakuza maendeleo ya kiwango cha juu ya ujumuishwaji wa kifedha na kujenga mfumo mzuri wa kifedha, ambao unaweza kubadilika kuendana na hali, wenye ushindani na unaojumuisha watu wote, ili kukidhi mahitaji ya kifedha ya watu na uchumi halisi.
Xi pia amesisitiza juhudi za kutoa mafunzo kwa idadi kubwa ya watu wanaofanya utafiti wa msingi wanaohitajika haraka kwa maendeleo ya China yanayotokana na uvumbuzi, na kuhimiza makampuni yanayomilikiwa na serikali kuboresha mifumo yao ya uvumbuzi na kuendeleza vyanzo vya teknolojia halisi za China.
Mkutano huo umetoa wito wa kuunga mkono na kuelekeza makampuni yanayoongoza katika viwanda na yale yanayomiliki teknolojia muhimu kupanua mageuzi na kuimarisha uvumbuzi, na kuhimiza juhudi za kuunga mkono makampuni ya biashara katika kubadilisha faida za soko kubwa zaidi la China kuwa faida ya ushindani wa kimataifa.
Li Keqiang, Wang Huning na Han Zheng, ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na manaibu wakuu wa Kamati Kuu ya kuimarisha mageuzi, wamehudhuria mkutano huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma