Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China lajiandaa kwa mkutano wake wa mwaka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 02, 2022

Wang Yang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), akihudhuria mkutano wa ufunguzi wa kikao cha 20 cha Kamati ya Kudumu ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 1, 2022. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Kamati ya Kudumu ya Kamati ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) imekutana Beijing siku ya Jumanne wiki hii kujiandaa kwa mkutano wake wa mwaka wa chombo hicho cha juu cha mashauriano ya kisiasa.

Wang Yang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya CPPCC, amehudhuria mkutano huo wa ufunguzi wa kikao cha 20 cha Kamati ya Kudumu ya Kamati ya 13 ya Taifa ya CPPCC.

Uamuzi wa kuitisha kikao cha tano cha Kamati ya Taifa ya 13 ya CPPCC kuanzia Machi 4 mjini Beijing ulithibitishwa na kupitishwa kwenye mkutano huo. Uamuzi huo pia unahusu ajenda zilizopendekezwa kwa mkutano wa mwaka.

Kikao hicho pia kimesikiliza na kupokea maelezo kuhusu rasimu ya ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya Kamati ya Taifa ya CPPCC na ripoti ya jinsi Kamati ya Kudumu imeshughulikia mapendekezo yaliyotolewa na washauri wa kisiasa, pamoja na mambo mengine.

Pia imesikiliza na kupokea ripoti kuhusu kazi ya kamati maalum za Kamati ya Taifa ya CPPCC na ripoti kuhusu mambo ya utumishi ya chombo hicho cha ushauri wa kisiasa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha