Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China lamaliza kikao cha kamati ya kudumu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 03, 2022

Wang Yang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), akizungumza wakati akiongoza mkutano wa kufunga kikao cha 20 cha Kamati ya Kudumu ya 13 ya CPPCC mjini Beijing, Machi 2, 2022. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Kamati ya Kudumu ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), chombo cha juu cha maushauriano ya kisiasa cha China, imefunga kikao chake cha 20 cha kamati ya kudumu Jumatano wiki hii hapa Beijing.

Wang Yang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China, aliongoza mkutano huo na kutoa hotuba.

Wang amedhihirisha kuwa katika mwaka uliopita, wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la umma la China walifanya mashauriano kwa msisitizo wa kufikia mwanzo mzuri wa kipindi cha Mpango wa 14 wa Maendeleo ya Miaka Mitano (2021-2025) na kuonesha wazi nguvu bora ya chombo hicho maalum cha mashauriano katika mfumo wa utawala wa nchi ya China.

Mkutano huo umejadili na kupitisha rasimu ya ajenda na ratiba ya mkutano wa 5 wa mwaka wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la umma la China, na ripoti kuhusu kazi ya Kamati ya Kudumu ya baraza hilo la CPPCC na jinsi inavyoshughulikia maoni na mapendekezo. Nyaraka hizo zitawasilishwa na kuthibtiishwa kwenye mkutano wa mwaka utakaofunguliwa siku chache zijazo.

Wang amesisitiza kuwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya baraza hilo wanapaswa kujiandaa kikamilifu kutoa ushauri na kujenga maelewano wakati wa kikao kijacho.

Amewataka wajumbe hao kubeba jukumu kubwa la kutoa ushauri wa kisiasa, kujitahidi kujibu maswali, kutatua masuala kwa kutumia uzoefu na utendaji wao wenyewe kazini, huku wakihakikisha mkutano wa mwaka unapangwa vizuri.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha