Kuwapatia urahisi wanavijiji katika usafiri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 03, 2022

Bw. Feng Bing akieleza kuhusu mji wa kale wa Datong.(Xinhua/Mpiga picha: Wu Yinbing)

Baada ya abiria kukaa kwenye viti ndani ya basi, dereva Feng Bing wa Kampuni ya mawasiliano ya umma ya Datong, Shanxi, ambaye ni mjumbe wa Bunge la Umma la China ambaye alitumia kipaza sauti akiwaeleza abiria kuhusu vivutio vya Pango la Yungang, Ukuta wa Jiulong, Hekalu la Huayan na mabaki mengine ya kale ya kitamaduni , na kuwaongoza abiria kuanza safari katika "mji mkuu wa kale".

  

Mandhari ya Mji wa Datong wakati wa baada ya kuaguka theleji. (Xinhua/Mpiga picha: Zhao Wengui)

 

  

Feng Bing anakula huku akitazama muda kwenye ratiba ya safari. (Xinhua/Mpiga picha: Wu Yinbing)

“Dereva wa basi anatakiwa kutazama hali ya barabarani, kuwahudumia abiria na pia kuwa tayari kukabiliana na hali ya dharura.” Tangu kuchanguliwa kuwa mjumbe wa Bunge la Umma la China Mwaka 2018, maoni na mapendekezo ya Feng Bing ya kila mwaka yanahusu madereva wa mabasi, Kwa mfano, alishauri kuwaweka madereva wa mabasi katika orodha ya watu wanaofanya kazi maalum.

Feng Bing ni mjumbe wa Bunge la Umma la China ambaye kazi yake ni kuendesha basi, kama watu wakitaka kumtafuta, wanachotakiwa ni kusubiri kwa safari chache tu za basi lake. “Lakini wakati ninapoendesha basi, siwezi kuzungumza nao, hivyo ninawafanya wasubiri katika ofisi yangu.”

  

Feng Bing akipokea simu za wananchi katika ofisi yake. (Xinhua/Mpiga picha: Wu Yinbing)

Ili kusikiliza maoni ya watu kwa urahisi zaidi, Feng Bing anatumia simu ya ofisi yake na mtandao wa kijamii wa WeChat kukusanya maoni ya watu.

Akizungumzia kuhusu mapendekezo yake ya kuleta kwenye Mkutano wa Bunge la Umma la China mwaka huu, Feng Bing alisema kuwa atatoa pendekezo kuhusu usafiri wa abiria wa vijijini, anapendekeza kuuunganisha mfumo wa usafiri wa abiria wa mabasi mijini na vijijini ili kuwafanya watu wote wafurahie kupata huduma ya usafiri wa mabasi yenye bei nafuu na urahisi.

Feng Bing ameandika maoni na mapendekezo kwenye daftari lake.

“Nikiwa mjumbe wa Bunge la Umma la China, inanibidi kustahili kuaminiwa na watu.” Feng Bing alipitia daftari ambalo alitumia kuandika maoni na mapendekezo ya miaka mingi iliyopita, akitumai kwamba kwenye mkutano wa Mwaka 2022, maoni na mapendekezo mengi mazuri yanayoendana na na mahitaji ya umma na kuweza kuondoa matatizo ya watu yatawasilishwa. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha