

Lugha Nyingine
Uchumi, Janga la UVIKO-19 na Demokrasia: ujumbe muhimu kutoka mkutano wa kuelekea "Mikutano Mikuu Miwili" ya China
Guo Weimin (wa pili kutoka kulia), Msemaji wa Mkutano wa 5 wa Kamati ya Taifa ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), akijibu maswali kwa njia ya video kutokana na mahitaji ya kuzuia na kudhibiti UVIKO-19 wakati wa mkutano na waandishi wa habari hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 3, 2022. (Xinhua/Yin Genge)
BEIJING - Guo Weimin, Msemaji wa Mkutano wa 5 wa Kamati ya Taifa ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) Alhamisi wiki hii ameelezea imani kubwa ya China katika hali ya uchumi, akisisitiza umuhimu wa sera ya “maambukizi sifuri ya UVIKO” ya China na kukosoa demokrasia ya Marekani, wakati China inaingia msimu wa mikutano mikuu miwili ya mwaka.
Guo Weimin, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari wa kabla ya "mikutano mikuu miwili" ya mwaka ya China kwamba, misingi ya muda mrefu ya uchumi wa China bado ni imara na haijabadilika.
Guo akijibu maswali ya waandishi wa habari amesema kuwa, uchumi wa China uliendelea kuimarika mwaka jana, na Pato la Taifa (GDP) lilipanda kwa asilimia 8.1 hatua kwa hatua.
Huku akikiri uwepo wa changamoto kubwa zinazoikabili China kutokana na mazingira magumu zaidi na yasiyo ya uhakika ya kimataifa, Guo amesema wajumbe na wataalam wa Kamati ya Taifa ya CPPCC wana imani kuwa China ina uwezo na mazingira wezeshi ya kufikia maendeleo ya uchumi imara, wenye kukua vizuri na ulio endelevu.
Guo amesema, China itaendelea kuchukua hatua madhubuti kufungua mlango kwenye kiwango cha juu na kufanya kazi kuchagia uchumi wa Dunia ulio wazi.
Ameongeza kwamba, uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja wa China Bara, katika matumizi halisi, ulifikia rekodi ya juu Mwaka 2021, hali ambayo inaonyesha imani ya wawekezaji wa kimataifa katika sera za ufunguaji mlango za China, mazingira ya biashara na matarajio ya maendeleo.
Mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China utafunguliwa leo Ijumaa mjini Beijing na kuhitimishwa Machi 10. Na Mkutano wa 5 wa Bunge la Umma la China utafunguliwa kesho Jumamosi.
Waandihsi wa Habari wakishiriki kwa njia ya video kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Mkutano wa 5 wa Kamati ya Taifa ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) mjini Beijing, Machi 3, 2022. (Xinhua/Li Xin)
Sera Sahihi
Katika mkutano na waandishi wa habari wa Jana Alhamisi, Guo amesisitiza kwamba sera ya China ya “maambukizi sifuri ya UVIKO” imesaidia kuleta uthabiti kwenye utendakazi wa minyororo ya viwanda na ugavi ya kimataifa.
"Hivi karibuni, baadhi ya maoni ya kimataifa yalisema kuwa mbinu ya China ya kukabiliana maambukizi ya UVIKO-19 imeathiri sekta ya viwanda na ugavi duniani, maoni ambayo nadhani si sahihi," amesema.
Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa jumla ya thamani ya biashara ya bidhaa za China ilipanda kufikia kiwango cha juu Mwaka 2021, ikizidi dola za kimarekani trilioni 6 ikiwa ni kwa mara ya kwanza, licha ya janga la UVIKO-19 kuendelea kuathiri biashara ya kimataifa.
Demokrasia haihodhiwi
Msemaji huyo pia amekosoa demokrasia ya Marekani, akisema kuwa Marekani inatumia demokrasia kama kisingizio cha kutumikia maslahi yake binafsi.
Guo wakati akijibu swali kuhusu iwapo China na Marekani zinapigania kuwa na ushawishi mkubwa zaidi wa kidemokrasia, amesema kwamba, madhumuni ya Marekani kuitisha kile kinachoitwa "Mkutano wa Kilele wa Demokrasia" ni kukandamiza nchi nyingine, kugawanya Dunia huku ikidumisha umwamba wake.
"Demokrasia kiasili ipo ya aina tofauti, na siyo hataza inayohodhiwa na nchi chache," Msemaji huyo amesema. "Mifumo ya kidemokrasia ya nchi inapaswa kuchaguliwa kwa uhuru na watu wa nchi husika kulingana na hali ya kitaifa."
Guo amekosoa baadhi ya nchi za Magharibi kulazimisha mifumo yao ya kidemokrasia kwa nchi nyingine kupitia "mapinduzi ya rangi," ambayo yamesababisha balaa kubwa.
Pia amepongeza demokrasia ya mchakato mzima wa watu ya China na majukumu ambayo CPPCC imetekeleza katika kuwezesha kufanya maamuzi ya kisayansi na kidemokrasia kupitia mashauriano, usimamizi, ushiriki na ushirikiano.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma