

Lugha Nyingine
Mkutano wa Bunge la Umma la China utafanyika kwa siku sita na nusu
Waandishi wa Habari wakishiriki mkutano wa vyombo vya habari kwa njia ya video kuhusu Mkutabo wa 5 wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC) mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 4, 2022. (Xinhua/Chen Zhonghao)
BEIJING - Mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China utafunguliwa kesho Jumamosi asubuhi hapa Beijing, msemaji wa Bunge hilo Zhang Yesui amesema leo Ijumaa.
Mkutano wa 5 wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC) umepangwa kukamilika Machi 11, ukiwa na ajenda 10, msemaji huyo ameuambia mkutano na waandishi wa habari.
Zhang amesema, wajumbe watapitia na kuthibitisha nyaraka mbalimbali zikiwemo ripoti ya kazi ya serikali na kujadili rasimu ya marekebisho ya Sheria ya Msingi ya Mabunge ya Umma ya ngazi za Serikali za Mitaa na Serikali za Umma za Mitaa.
Zhang pia amesema, wajumbe watajadili na kuthibitisha rasimu ya uamuzi kuhusu idadi ya wajumbe wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC ya 14) na uchaguzi wao, na rasimu mbili za namna Mikoa ya Utawala Maalum ya Hong Kong na Macao itachagua wajumbe wao kwa NPC ya 14.
Zhang Yesui (Katikati), Msemaji wa Mkutano wa 5 wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC), akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kupitia njia ya video mjini Beijing, Machi 4, 2022. Mkutano huo na waandishi wa habari ulifanyika kwa njia ya video kutokana na mahitaji ya kuzuia na kudhibiti UVIKO-19. Zhang amejibu maswali kutoka kwa vyombo vya habari kuhusu ajenda za mkutano wa 5 wa Bunge la umma la China na kazi za wajumbe wa Bunge la Umma. (Xinhua/Chen Yehua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma