Mjumbe wa Bunge la Umma la China anayejikita katika kuendeleza kazi za mikono za China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 05, 2022

Hou Zhanying, msanifu wa Sanaa za mikono mwenye uzoefu, ambaye ni Mjumbe wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC), amejitolea kuunganisha umaalumu wa utamaduni wa China katika kazi zake za usanifu wa Sanaa za mkono. Mwaka huu, atawasilisha maoni na mapendekezo kuhusu maendeleo endelevu ya tasnia ya kazi za mikono kwenye mkutano wa Bunge la Umma la China unaofanyika hapa Beijing, Mji Mkuu wa China.

Hou, Mkuu wa Idara ya Usanifu wa Kampuni ya Vidani ya Beijing Orafi amesanifu na kutengeneza medali na zawadi mbalimbali za taifa nchini China, pamoja na mapambo ya kila siku, akishirikiana na timu yake. Mfano mmoja ni zawadi za taifa zilizotolewa kwa wenzi wa viongozi wa kigeni katika Kongamano la Ushirikiano wa Kimataifa la “Ukanda Mmmoja, Njia Moja” Mwaka 2017. Ni kisanduku chavito cha mtindo wa China, Sanaa hii ya mikono inaunganisha ufundi wa jadi wa China kama vile kuchonga vichanio vya nywele na kuchora kwa uchapishaji wa 3D. . "Zawadi ya Taifa lazima iwe na utamaduni wa China na sura ya China," Hou amesema. "Muundo na utengenezaji wake lazima uonyeshe umaalumu wa utamaduni wa China," ameongeza.

Imani yake juu ya utamaduni wa China imeongezeka katika mchakato wa kusanifu sanaa za mikono"Mimi na timu yangu, tuko tayari kuhimiza maendeleo endelevu ya kazi za sanaa za mikono na kuzifanya zioneshe utamaduni wa China ulioendelea kwa maelfu ya miaka," anasema.

Hou anaamini kuwa uvumbuzi ni muhimu ili kuzifanya kazi za mikono zenye umaalumu wa China kwenda duniani kote, na mitindo ya kisasa inaweza kuongeza uhai zaidi katika kazi za sanaa za mikono za kitamaduni.

Hou, ambaye yuko katika mwaka wake wa mwisho wa awamu ya miaka mitano ya mjumbe wa NPC ya 13, sasa anafahamu kazi yake ya kisiasa, lakini bado anahisi kusongwa na mawazo kwa namna fulani. "Ninatoka mstari wa mbele, kwa hivyo maoni na mapendekezo yangu lazima yaonyeshe hali halisi na kusaidia kukabiliana na changamoto katika shughuli zetu . Wajumbe wenzangu wote ni wawakilishi kutoka hali mbalimbali za maisha, na maoni yao yote ni ya kitaalamu sana. Lazima nifanye kazi bila kuchoka ili kujiboresha,” amesema.

Hou ana maoni na mapendekezo mawili kwenye mkutano wa Bunge la Umma la China, ujenzi wa chapa ambayo inazingatia zaidi kuziba pengo la mwisho katika kuondoa vizuizi vya kurithisha utamaduni usioshikika na kuhimiza uhai na maendeleo endelevu ya biashara za sanaa na usanifu wa viwango vya juu, na kuandaa vipaji wenye sifa ya juu kwa ajili ya sekta hiyo.

Hou anaamini kuwa vijana wengi zaidi watajitokeza katika shughuli za usanifu wa sanaa ya mikono katika siku zijazo. "Vijana wengi wanapenda utamaduni wa jadi wa China, na watajivunia kazi hii. Tunaorithi siyo ufundi wa kazi tu, bali pia ni ustaarabu ulioendelea kwa maelfu ya miaka." 

Hou Zhanying, msanifu wa sanaa za mikono mwenye uzoefu, ambaye ni mjumbe wa Mkutano wa 5 wa Bunge la Umma la 13 la China. (People's Daily Online/Yuan Meng)

Picha iliyopigwa Februari 28, 2022 inaonyesha "Maelewano chini ya Pepo: Kisanduku cha kuhifadhi vidani" kilichosanifiwa na kutengenezwa na timu ya Hou. (People's Daily Online/Yuan Meng)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha