Ripoti ya kazi ya serikali ya China: soko kubwa la wazi litatoa fursa zaidi kwa makampuni kutoka duniani kote

(CRI Online) Machi 05, 2022

Ripoti ya kazi ya serikali ya China kwa mwaka 2022 iliyowasilishwa kwenye mkutano wa bunge la umma tarehe 5, imeeleza kutumia kikamilifu mitaji ya kigeni, na kufungua soko kubwa la China, jambo ambalo hakika litatoa fursa zaidi kwa makampuni kutoka nchi zote kujiendeleza nchini China.

 Ripoti hiyo imeeleza kuwa ni muhimu kupanua maeneo yanayoruhusiwa kuwekezwa na nchi za nje, na kuunga mkono mitaji ya kigeni kuwekezwa katika sera za uzalishaji wa hali ya juu na kati, utafiti na maendeleo, huduma za kisasa, na vile vile katika mikoa ya kati magharibi, na kaskazini mashariki.

 Ripoti pia imesisitiza kuwa China inapenda kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na nchi nyingine duniani ili kupata maendeleo kwa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha