Viongozi wa China wajumuika na washauri wa kisiasa kwenye mijadala ya vikundi

(CRI Online) Machi 07, 2022

Viongozi waandamizi wa China jumapili walijumuika na washauri wa kisiasa wa taifa kwenye mijadala ya vikundi tofauti katika Mkutano wa tano wa Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC).

Viongozi hao wakiwemo pamoja na waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang, wote ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Akishiriki kwenye majadiliano ya kikundi cha washauri wa kisiasa wa taifa kutoka sekta ya uchumi, Waziri Mkuu Bw. Li Keqiang alisema China itadumisha viashiria vikuu vya uchumi kwenye viwango vinavyofaa, kutokana na umuhimu wake kwa utulivu na maendeleo ya kiuchumi katika muda mrefu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha