Rais Xi Jinping asisitiza umuhimu wa upatikanaji wa bidhaa za kilimo, na kujenga mfumo madhubuti wa huduma za jamii

(CRI Online) Machi 07, 2022

(Picha inatoka CRI.)

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kuzingatia ipasavyo kuboresha uwezo wa uzalishaji wa kilimo, na kuendelea na juhudi za kuhimiza maendeleo ya kiwango cha juu ya huduma za jamii.

Rais Xi amesema hayo alipokutana na washauri wa kisiasa wa taifa kutoka sekta za kilimo na huduma za jamii walioko Beijing kuhudhuria mkutano wa Baraza la mashauriano ya kisasa la China (CPPCC).

Rais Xi ameshiriki kwenye mijadala ya wajumbe wa sekta hizo, ambapo alisikiliza maoni na mapendekezo yao. Rais Xi amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha upatikanaji wa mazao muhimu ya kilimo, hasa nafaka, kuwa ni kipaumbele katika kuendeleza vijiji.

Rais Xi kwa niaba ya Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China pia ametoa salamu za kila la heri za siku ya kimataifa ya wanawake, kwa wanawake wa makabila yote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha