Waziri Mkuu wa China asisitiza kuhakikisha kwa hatua madhubuti maendeleo mazuri na endelevu ya kiuchumi na kijamii

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 07, 2022

BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Keqiang Jana Jumapili amesisitiza kufanya juhudi za pamoja na kwa hatua madhubuti ili kuhakikisha maendeleo mazuri na endelevu ya kiuchumi na kijamii.

Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akishiriki kwenye majadiliano ya kikundi cha wajumbe wa Mkoa unaojiendesha wa Guangxi kwenye Mkutano wa Tano cha Bunge la Umma la 13 la China mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 6, 2022. (Xinhua/Ding Haitao)

Li, pia Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ameyasema hayo aliposhiriki kwenye majadiliano ya kikundi cha wajumbe wa Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi kwenye Mkutano wa Tano wa Bunge la Umma la 13 la China unaoendelea hapa Beijing.

Li amekiri kwamba maendeleo ya China yanaweza kukabiliwa na matatizo na changamoto zaidi mwaka huu, na kuutaka Mkoa wa Guangxi kutumia vyema sera husika zinazounga mkono mkoa huo, na kutumia nguvu yake bora ili kujipatia maendeleo bora zaidi.

Amesema kwamba, Mkoa wa Guangxi unapaswa kuchukua fursa ya utekelezaji wa makubaliano ya Uwenzi Kamili wa Kiuchumi wa Kikanda ili kukuza ushirikiano wake na Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki.

Li amesisitiza umuhimu wa kurejesha kodi zilizotozwa na kupunguzwa kwa ushuru katika kuimarisha uhai wa wadau wa soko, akisisitiza kwamba sera hizi zinapaswa kulenga kunufaisha moja kwa moja wadau wa soko na urejeshaji huo wa kodi unapaswa kuweka kipaumbele kwa biashara ndogo na za ukubwa wa kati kwa msisitizo zaidi katika kusaidia sekta ya viwanda.

Kuhusu kuhakikisha na kuboresha hali ya maisha ya watu, Li ametoa wito wa kuongezwa kwa juhudi za kuendelea kuimarisha elimu ya lazima, kuboresha huduma za matibabu katika ngazi ya mashina , na kuendeleza ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha