Nchi takriban mia moja zaunga mkono pendekezo la maendeleo ya dunia

(CRI Online) Machi 08, 2022

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema, pendekezo alilotoa rais Xi Jinping kuhusu maendeleo ya dunia linalingana na mahitaji ya pande zote, ambalo limeungwa mkono haraka na Umoja wa Mataifa pamoja na nchi karibu mia moja. Amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na nchi zote katika kutekeleza vizuri pendekezo hilo muhimu, na kutoiacha nyuma nchi yoyote, ili kujenga kwa pamoja Jumuiya ya Maendeleo ya Pamoja ya Dunia.

Wang Yi ameeleza kuwa wazo kuu la Pendekezo la Maendeleo ya Pamoja, kiini chake ni maslahi ya wananchi, ambalo lengo kuu ni kuchangia utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030.

Wang pia amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na pande zote, kufuatilia zaidi matatizo makubwa yanayozikabili nchi zinazoendelea kama vile kupunguza umaskini, usalama wa chakula, ufufukaji wa uchumi, ajira na mafunzo, elimu na afya, na maendeleo ya kijani, na kuchangia katika kutimiza malengo 17 ya maendeleo endelevu mwaka 2030. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha