Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China lafanya kikao cha pili katika mkutano wa mwaka

(CRI Online) Machi 08, 2022

(Picha inatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), likiwa ni chombo cha ngazi ya juu cha kutoa ushauri wa kisiasa nchini China, jana Jumatatu lilifanya kikao cha pili katika mkutano wake wa mwaka.

Bw. Wang Yang, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa kamati ya taifa ya baraza hilo, alihudhuria mkutano huo. Wajumbe 12 wa kamati ya taifa ya baraza hilo walitoa maoni yao kwenye mkutano huo.

Bw. Ge Huijun, ambaye ni mmoja wa wajumbe hao, alitoa wito kwa washauri wa kisiasa kubeba majukumu yao na kutekeleza kwa moyo wote demokrasia ya kushauriana ya kijamaa.

(Picha inatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

(Picha inatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha