

Lugha Nyingine
Bunge la Umma la China lafanya kikao cha pili cha Mkutano wa Mwaka
Li Zhanshu, Spika wa Bunge la Umma la China (NPC) akitoa ripoti ya kazi ya Kamati ya NPC kwenye kikao cha pili cha Mkutano wa Tano wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC ya 13) katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, mjini Beijing , Machi 8, 2022. (Xinhua/Liu Weibing)
BEIJING – Mkutano wa Tano wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC), umefanya kikao chake cha pili leo Jumanne.
Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na viongozi wengine wa China wamehudhuria mkutano huo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.
Li Zhanshu, Spika wa Bunge la Umma la China (NPC), ametoa ripoti ya kazi ya Kamati ya NPC kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa NPC wamesikiliza na kuthibitisha ripoti ya kazi ya Mahakama Kuu ya Umma ya China iliyotolewa na Mkuu wake Zhou Qiang na ripoti ya kazi ya Idara Kuu ya Uendesha Mashtaka ya Umma ya China iliyotolewa na Mwendesha Mashtaka Mkuu Zhang Jun.
Wang Chen akiongoza kikao cha pili cha Mkutano wa Tano wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC) kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, hapa Beijing, Machi 8, 2022. (Xinhua/Shen Hong)
Zhou Qiang, Mkuu wa Mahakama Kuu ya Umma ya China (SPC), akitoa ripoti ya kazi ya SPC kwenye kikao cha pili cha Mkutano wa Tano wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC ya 13) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 8, 2022. (Xinhua/Shen Hong)
Zhang Jun, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Idara Kuu ya Uendesha Mashtaka ya Umma ya China (SPP), akitoa ripoti ya kazi ya SPP katika kikao cha pili cha Mkutano wa Tano wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC ya 13) kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, hapa Beijing, Machi 8, 2022. (Xinhua/Shen Hong)
Kikao cha pili cha Mkutano wa Tano wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC ya 13) unafanyika kwenye Jumba la Mikutano la Beijing, Machi 8, 2022. (Xinhua/Xing Guangli)
Kikao cha pili cha Mkutano wa Tano wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC ya 13) unafanyika kwenye Jumba la Mikutano la Beijing, Machi 8, 2022. (Xinhua/Xing Guangli)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma