Rais Xi Jinping asisitiza kusimamia jeshi kwa mujibu wa sheria

(CRI Online) Machi 08, 2022

(Picha inatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kusimamia jeshi kwa mujibu wa sheria na kuhimiza utawala wa sheria kwenye ulinzi wa taifa na ujenzi wa jeshi.

Rais Xi amesisitiza hayo alipokutana na wajumbe wa jeshi la ukombozi wa umma na wa jeshi la polisi, kwenye mkutano wa tano wa bunge la umma la 13 la China unaoendelea mjini Beijing. Rais Xi amepongeza mafanikio yaliyopatikana kwenye usimamizi wa jeshi kwa mujibu wa sheria baada ya juhudi za miaka mingi toka mwaka 2012 ulipofanyika mkutano mkuu wa Chama cha kikomunisti cha China.

Rais Xi amesema katika kusimamia jeshi kwa mujibu wa sheria, mkazo unatakiwa kuwekwa kwenye kuunda jeshi la kimapinduzi, la kisasa na lenye vigezo, na kujenga mfumo wa China wa kusimamia mambo ya jeshi kwa mujibu wa sheria.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha