

Lugha Nyingine
Elewa ‘Demokrasia ya mchakato mzima wa Umma’ ya China katika "mikutano mikuu miwili"
Wajumbe wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC) wakihudhuria kikao cha pili cha Mkutano wa Tano wa NPC ya 13 kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 8, 2022. (Xinhua/Liu Weibing)
BEIJING - Demokrasia ya mchakato mzima wa Umma ya China, imeundwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika kuwaongoza watu kutafuta demokrasia, kuendeleza demokrasia na kutimiza demokrasia, inaonesha dhana mpya ya CPC katika kuendeleza nadharia ya demokrasia, kuanzisha mifumo ya kidemokrasia na kufanya uzoefu nchini China.
"Mikutano Mikuu Miwili" inayoendelea nchini China, yaani mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China (NPC) na mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC), inawapa watazamaji fursa ya kufahamu wazo na utekelezaji wa ‘Demokrasia ya mchakato mzima wa Umma’ ya China, dhana hii imekuwa gumzo kwenye jukwaa la kisiasa la China katika miaka iliyopita.
Katika kipindi cha takriban wiki moja, karibu Wajumbe 3,000 wa Bunge la Umma la China na karibu wajumbe 2,000 wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China wanatekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya sheria na mapitio, majadiliano, uthibitishaji wa mfululizo wa ripoti za kazi, kwa nia ya kupata msingi wa pamoja na kukubaliana kwa maslahi ya watu wa China.
Ikiwa ni dhana mpya katika zama mpya, Demokrasia ya mchakato mzima wa Umma’ ya China inatokana na urithi tajiri wa mazoea ya kidemokrasia ya CPC tangu kuanzishwa kwake. Moja ya mifano ya kielelezo ya CPC ya kuhamasisha watu wa vijijini kutekeleza haki zao za kupiga kura, ambapo wanavijiji walitumia njia ya kuweka maharage kwa kuchagua wajumbe wao wakati wa mapinduzi.
Dhana hiyo ina misemo miwili muhimu: "mchakato mzima," na "demokrasia ya umma."
"Demokrasia ya Umma" ni maisha ya kijamaa. Asili ya demokrasia ya ujamaa ni kwamba watu ndiyo mabwana wa nchi. Imeainishwa katika Katiba ya Nchi ya China kwamba mamlaka yote nchini ni ya wananchi, na watu wa China wanashiriki kwa mujibu wa sheria na kwa namna mbalimbali katika mambo ya utawala wa serikali, mambo ya uchumi na utamaduni, na masuala ya kijamii.
"Mchakato mzima" maana yake ni kwamba watu wanashiriki katika uchaguzi wa kidemokrasia, kufanya mashauriano, kufanya maamuzi, usimamizi na uangalizi kwa mujibu wa sheria.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma