Timu ya China yapata medali mbili za dhahabu tena kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 10, 2022

Machi 9, Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ilifikia siku yake ya tano ya mashindano. Kwenye mashindano ya mbio za nyika za kuteleza kwenye theluji kwa kutumia magongo (kwa kukaa) ya michezo hiyo ya Olimpiki, Zheng Peng na Yang Hongqiong walishinda medali za dhahabu kwa Mbio za nyika za kuteleza kwenye theluji kwa kukaa kwa wanaume na kwa wanawake. Timu ya China imeendelea kuchukua nafasi ya kwanza kwa idadi ya medali za dhahabu na medali zote kwa kuwa na medali za dhahabu 10, medali za fedha 9 na medali za shaba 12.

Mchezaji wa Timu ya China Zheng Peng (kushoto) na mwenzake Mao Zhongwu walipata medali ya dhahabu na ya fedha katika mchezo wa mbio za nyika za kuteleza kwenye theluji kwa kukaa kwa wanaume kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing Machi 9. (Xinhua/ Mpiga picha:Li Bo)

Mchezaji wa Timu ya China Zheng Peng alipata medali ya dhahabu katika mchezo wa mbio za nyika za kuteleza kwenye theluji kwa kukaa kwa wanaume kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing Machi 9. (Xinhua/ Mpiga picha:Li Bo)

Zheng Peng alitwaa medali ya dhahabu kwenye mashindano ya mbio za nyika za kuteleza kwenye theluji kwa kukaa kwa wanaume akitumia muda wa dakika 2 na sekunde 42.4, mchezaji mwingine wa Timu ya China Mao Zhongwu alipata medali ya fedha kwa kutumia muda wa dakika 2 na sekunde 44.9 na mchezaji kutoka Timu ya Canada Collin Cameron alipata medali ya shaba. Jambo linalostahili kuelezwa ni kuwa hii ni medali ya pili ya dhahabu kwa Zheng Peng kwenye Michezo hii ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya baridi, na pia amekuwa mwanamichezo wa kwanza wa kiume wa China kushinda medali mbili za dhahabu kwenye Michezo ya Walemavu ya Majira ya baridi.

Mchezaji wa Timu ya ChinaYang Hongqiong alitwaa medali ya dhahabu katika Mbio za nyika za kuteleza kwenye theluji kwa kukaa kwa wanawake kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing Machi 9. (Xinhua/ Mpiga picha:Li Bo)

Mchezaji wa Timu ya ChinaYang Hongqiong alitwaa medali ya dhahabu katika Mbio za nyika za kuteleza kwenye theluji kwa kukaa kwa wanawake kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing Machi 9. (Xinhua/ Mpiga picha:Li Bo)

Yang Hongqiong alipata medali ya pili ya dhahabu ya michezo hiyo ya Olimpiki kwenye mchezo wa mbio za umbali mfupi za nyika za kuteleza kwenye theluji kwa wanawake (kwa kukaa). Yang alitwaa ushindi kwa kutumia dakika 3 na sekunde 18.3, mchezaji kutoka Marekani mwenye maarifa mengi veteran Oksana Masters alipata medali ya fedha, na mchezaji mwingine wa Timu ya China Li Panpan alipata medali ya shaba.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha