Mkutano wa 5 wa Bunge la Umma la 13 la China wafungwa

(CRI Online) Machi 11, 2022

(Picha inatoka CRI.)

Mkutano wa 5 wa Bunge la Umma la 13 la China umefungwa baada ya kumaliza ajenda mbalimbali. Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China na serikali ya China akiwemo Rais Xi Jinping wamehudhuria ufungaji wa mkutano huo.

Spika wa Bunge hilo Li Zhanshu amesema huu ni mwaka muhimu wa mchakato wa maendeleo ya mambo ya Chama cha Kikomunisti cha China na taifa la China, inapaswa kutekeleza kwa kina msingi wa Mkutano wa serikali kuu kuhusu kazi za Bunge la Umma, kutambua kwa kina majukumu mapya ya Bunge hilo katika mfumo wa utawala, na kuinua kiwango cha Bunge hilo la umma.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha