Rais wa IPC atangaza kufungwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 14, 2022

Andrew Parsons, Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu (IPC), akihutubia ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Walemavu ya Beijing 2022 kwenye Uwanja wa Taifa wa Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 13, 2022. (Xinhua/Wu Zhuang)

BEIJING - Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Paralimpiki (IPC) Andrew Parsons Jana Jumapili jioni ametangaza kufungwa rasmi kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Walemavu ya Beijing 2022.

Katika hotuba yake wakati wa sherehe ya ufungaji iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Beijing, Parsons amesema kuwa michezo hiyo imekuwa mwanga mpya kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Walemavu.

"Uratibu wa kustaajabisha, viwanja bora na michezo ya kuvutia - alama kuu ya Michezo bora hapa Beijing. Kwa hakika, China imeweka kiwango cha juu kwa Michezo yote ya Majira ya Baridi katika siku zijazo. Kwa hakika, China sasa ni nchi yenye nguvu ya michezo ya majira ya baridi," amesema mkuu huyo wa IPC.

Beijing ni mji wa kwanza kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya joto na Baridi. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha