Mafanikio ya Michezo ya Olimpiki na Paralimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing yanadhihirisha moyo wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu - wataalam

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 15, 2022

BEIJING - Wakati Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Walemavu ya Beijing 2022 ilipofungwa hapa Beijing Jumapili ya wiki iliyopita, China imetimiza ahadi yake kwa Dunia, na kutoa mchango mpya kwa malengo ya kimataifa ya Olimpiki.

Wataalamu kutoka sehemu mbalimbali za Dunia wameeleza kushukuru kwao kwa juhudi za China katika suala hilo, wakisisitiza kwamba mafanikio ya Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya baridi ya Beijing yanadhihirisha moyo wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

Mshauri wa zamani wa masuala ya utalii wa Misri katika Mji wa Beijing Nasser Abdel-Aal amesema, China imefanya kila juhudi kukabiliana na athari za janga la UVIKO-19 ili kufanya Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya baridi ya Beijing kuwa matukio ya kimataifa ya michezo, ambayo siyo tu yanatimiza ahadi nzito ya China kwa jumuiya ya kimataifa, lakini pia imechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya malengo ya kimataifa ya Olimpiki, kukuza maingiliano ya kitamaduni kati ya nchi na kuimarisha urafiki kati ya watu wa Dunia nzima.

Abdel-Aal ameongeza kuwa, mafanikio ya michezo hiyo yako wazi, yenye kutia hamasa na ushauri mkubwa sana kwa ajili ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

“Dunia kwa mara nyingine iliiona China inayowajibika”, amesema Zahid Farooq Malik, mhariri mkuu wa Daily Metro Watch, gazeti la Pakistan, akiongeza kuwa China imeonyesha Dunia "picha nzuri ya mshikamano wa binadamu."

Cavince Adhere, msomi wa masuala ya uhusiano wa kimataifa wa Kenya amesema, China imejizolea sifa kutoka kwa nchi mbalimbali duniani kwa kuandaa michezo hiyo kwa viwango vya kuvutia vya kiusalama na kimichezo pamoja na uwepo wa janga la UVIKO-19 duniani.

China imeonyesha maadili ya usawa, uvumilivu na kujiendeleza kupitia Michezo ya Olimpiki, ambayo Adhere anasema imeifanya China kuwa "nyumba ya fursa sawa kwa wote."

Liu Di, Profesa wa Chuo Kikuu cha Kyorin cha Japan, amesema michezo hiyo ya olimpiki na paralimpiki ya majira ya baridi ya Beijing imefanyika katika wakati mgumu usio na kifani, na moyo wa uanamichezo ulioonyeshwa kwenye michezo hiyo kwa hakika utaendelea kuwahamasisha watu kushikamana, kushirikiana na kupiga hatua kimaendeleo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha