AU yataka Afrika kunyakua nafasi ya soko la kidijitali linaloendelea kwa kasi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 16, 2022

ADDIS ABABA - Naibu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Monique Nsanzabaganwa amesema Afrika inapaswa kunyakua nafasi soko la kidijitali linaloendelea kwa akasi ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa na huduma katika bara zima

Nsanzabaganwa amesema hayo Jumanne wiki hii wakati Bara la Afrika lilipoungana na jumuiya ya kimataifa katika Maadhimisho ya 39 ya Siku ya Haki za Wateja Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka Machi 15 chini ya kaulimbiu ya "Upatikanaji sawa wa huduma za kifedha za Kidijitali."

"Kunyakua nafasi ya soko la kidijitali linaloendelea kwa kasi ni muhimu hasa katika Afrika ambapo upatikanaji wa bidhaa na huduma nyingi bado una vikwazo kwa walio wengi," Nsanzabaganwa amesema katika taarifa yake kuhusu Siku ya Haki za Wateja Duniani.

Huku akibainisha kuwa Bara la Afrika lina kiwango cha kupenya kwa mtandao cha asilimia 43, Nsanzabaganwa amesema uvumbuzi unabadili jinsi watu wanavyofanya malipo na kuishi maisha yao katika bara zima, akisisitiza kwamba huduma za kifedha za kidijitali na athari zake katika ujumuishaji wa kifedha na utulivu wa kifedha ni muhimu kwa maendeleo barani Afrika.

Nsanzabaganwa amebainisha kuwa Bara la Afrika linaongoza kwa idadi inayoongezeka ya usambazaji wa huduma za kifedha za kidijitali.

Ameonya kuwa watumiaji wa fedha za kidijitali wanazidi kukabiliwa na changamoto za ulaghai, kudanganywa, wizi wa data binafsi na upotovu wa data, ambao unachangiwa zaidi na janga la UVIKO-19.

Amesema idadi ya vijana inayoongezeka barani Afrika inaungana na Dunia ya kidijitali inayobadilika kila mara na ni muhimu kwa watoa maamuzi na watunga sera wa bara hili kutumia uzoefu huu kwa njia ambayo ni bora kwa vijana wa bara hili.

Nsanzabaganwa, hata hivyo, amesisitiza kuwa wanawake wa Afrika bado wana uwezekano mdogo wa kupata huduma rasmi za kifedha kuliko wanaume.

"Pesa kwa njia ya simu na uwezo wa kupokea pesa kwa urahisi na kwa usalama kutoka kwa mitandao ya kijamii imeonekana kuwa kivutio kwao na hivyo kusaidia kupunguza tofauti za kijinsia katika bara zima," amesema.

Wiki iliyopita, AU ilizindua Mpango wa Wanawake na Vijana wa Kifedha na Kiuchumi (WYFEI 2030), ambao ni mpango wa matokeo ya pamoja ambao unalenga kufikia mabadiliko ya kijamii kuhusiana na hali ya kifedha na kiuchumi na ushiriki wa wanawake na vijana barani Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha