Lugha Nyingine
Rais Xi ataka udhibiti wa haraka wa milipuko ya UVIKO-19 ya hivi karibuni nchini China
(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)
BEIJING - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Alhamisi wiki hii amehimiza kuzuia haraka kuenea kwa janga la UVIKO-19.
Xi ameyasema hayo alipokuwa akiongoza mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ili kuchambua hali ya janga la UVIKO-19.
Ameeleza kwamba, ufanisi wa kiuchumi wa China na mwitikio wa kudhibiti UVIKO-19, ambavyo vyote nchi hiyo imeongoza Dunia, umeonyesha kikamilifu nguvu na uwezo wa China katika kuzuia na kudhibiti janga. Pia umedhihirisha nguvu bora ya uongozi wa CPC na mfumo wa kijamaa.
"Ushindi unatokana na uvumilivu," Xi amesema. Amezitaka idara na sehemu zote kujiandaa kwa changamoto na ugumu katika kukabiliana na UVIKO-19 ndani na nje ya nchi.
“Watu wanapaswa kuwekwa mbele kila wakati” amesema Xi. Amesisitiza kuwa, ni lazima kushikilia hatua sahihi za kisayansi, na kushikilia kufuata sera ya ‘maambukizi sifuri ya UVIKO’ ili kuzuia kuenea kwa janga hilo kwa haraka zaidi.
Ametoa wito kwa uvumbuzi zaidi wa kisayansi na kiteknolojia katika utafiti na maendeleo ya chanjo, vifaa vya upimaji kwa haraka, na dawa, ili kuleta ufanisi katika kuzuia na kudhibiti janga.
Mkutano huo umezingatia maambukizi ya UVIKO-19 ya hivi majuzi katika makundi na maeneo mbalimbali, nayo yameonekana katika maeneo mengi nchini humu, yakienea kwa upana na kujirudia mara kwa mara, mkutano huo umetaka utekelezaji mkali wa sera ya kutambua mapema maambukizi, kuripoti mapema, kuweka karantini na kufanya matibabu mapema.
Mkutano huo umesisitiza kuwa, ni lazima kudumisha uzalishaji na ugavi wa vitu vya mahitaji ya kila siku na kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji ya watu ya matibabu.
Mkutano umetoa maagizo ya kuimarishwa kwa juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Korona kwenye maeneo ya mipakani hususani kwenye viwanja vya ndege na bandari ili kujenga ulinzi thabiti dhidi ya maambukizi yanayotoka nje ya nchi na kuimarishwa kwa hatua za kuzuia na kudhibiti maambukizi kwenye maeneo ya mashuleni na maeneo mengine muhimu kila siku kama kawaida.
Mkutano umesisitiza kwamba, juhudi kubwa zaidi zinapaswa kufanywa katika zoezi la uchanjaji wa chanjo dhidi UVIKO-19 na kuinua kiwango cha uchanjaji wa chanjo ili kuimarisha ulinzi dhidi ya janga.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma