Uwanja wa ndege wa kwanza wa kazi maalumu ya usafirishaji wa bidhaa wa China wamaliza majaribio ya kuruka kwa ndege

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 21, 2022

Ndege ya usafirishaji wa bidhaa iliyofanya majaribio ikiruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Huahu wa Mji wa Ezhou Machi 19. (Mpiga picha: Xiao Yijiu/Xinhua)

Kazi ya majaribio ya kuruka kwa ndege katika Uwanja wa Ndege wa Huahu wa Mji wa Ezhou ilimalizika kwa mafanikio Machi 19. Hii ni mara ya kwanza kwa China kufanya majaribio ya kuruka kwa ndege kwenye uwanja mpya, ambao unatumiwa na ndege za mizigo tu.

Kazi hiyo ya majaribio ilihusisha kuruka na kutua kwa ndege kwenye njia mbili za ndege za upande wa mashariki na upande wa magharibi kwa pande nne. Majaribio ya safari ya ndege yalihusisha kukagua na kupima utaratibu wa kuruka kwa ndege na mfumo wa kuongoza ndege , kukagua njia za ndege, alama za eneo la kuruka kwa ndege na majengo na vifaa vingine. Yalikuwa ni majaribio ya pande zote kwa uwezo wa jumla wa uhakikisho wa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Huahu wa Mji wa Ezhou. Hayo yote yana umuhimu mkubwa kwa kuzinduliwa kwa uwanja huo wa ndege mwishoni mwa Mwezi Juni wa Mwaka huu.

Uwanja wa Ndege wa Huahu wa Ezhou ni uwanja wa kwanza kwa Asia na wa nne duniani wa kazi maalum ya kusafirisha bidhaa Ulisanifiwa kukidhi mahitaji ya kusafirisha abiria milioni 1 na bidhaa na vifurushi vyenye tani milioni 2.45 ifikapo Mwaka 2025.

Kwenye uwanja huo wa ndege kuna kituo cha kupitisha mizigo chenye mita za mraba laki saba, jengo la abiria kusubiri ndege lenye mita za mraba elfu 15, na eneo lenye nafasi 124 kwa ndege kusimama, kupakia na kupakua mzigo. 

Uwanja wa Ndege wa Huahu wa Mji wa Ezhou na picha ilipigwa Machi 19. (Mpiga picha: Xiao Yijiu/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha