

Lugha Nyingine
Mji wa Shenzhen nchini China warejea kazi na uzalishaji wa kawaida baada ya Mlipuko mpya wa UVIKO-19
Wafanyakazi wakikagua taarifa za wakazi kwa ajili ya vipimo vya virusi vya Korona katika Wilaya ya Futian ya Shenzhen, Mkoa wa Guangdong nchini China, Machi 17, 2022. (Picha na Chu Yan/Xinhua)
SHENZHEN – Mamlaka ya mji wa Shenzhen jana imesema, ofisi za serikali, kampuni, na biashara katika mji huo zimepangwa kurejea kufanya kazi na shughuli za uzalishaji kama kawaida kuanzia leo Jumatatu wakati maambukizi ya hivi karibuni ya UVIKO-19 yakipungua.
Kwa mujibu wa waraka uliotolewa na idara ya kuzuia na kudhibiti UVIKO-19 ya Shenzhen, mji huo utaanza tena huduma za usafiri wa mabasi na treni za chini ya ardhi kuanzia leo Jumatatu.
Waraka unasema, mamlaka zinatoa hatua za kuhakikisha usalama na uthabiti wa minyororo ya uzalishaji na usambazaji, na utaratibu wa maisha na kazi kwa wakaazi.
Unaeleza kuwa, baada ya upimaji wa virusi vya Korona kwa mara tatu katika mji mzima tangu Machi 14, hali ya kuzuia na kudhibiti UVIKO-19 huko Shenzhen bado ina changamoto lakini kwa ujumla inaweza kudhibitiwa.
Waraka huo wa kuzuia na kudhibiti virusi vya Korona utaanza kutumika kuanzia Machi 21 hadi Machi 27.
Maeneo yasiyo ya lazima ya umma ya ndani, ikiwa ni pamoja na vyumba vya massage, vyumba vya mchezo wa karata na huduma za umma za mtandao, pamoja na huduma za watoto na taasisi za elimu nje ya mtandao, zitaendelea kufungwa. Migahawa yote itafanya kazi kwa nusu ya uwezo.
Waraka huo umeagiza kutekelezwa kwa hatua tofauti za kukabiliana na UVIKO-19 kwa makampuni yanayohusika na minyororo ya uzalishaji na usambazaji bidhaa, ili kuhakikisha usalama na utulivu wa minyororo hii.
Kwa mujibu wa waraka, mamlaka katika wilaya zote na idara zinazohusika zinahitaji kuimarisha juhudi za kutoa huduma zinazolengwa kwa makampuni ya biashara, kukabiliana haraka na mahitaji yao, na kuwasaidia kuondokana na matatizo yao ya uzalishaji na uendeshaji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma