Faida za viwanda za China zaongezeka kwa asilimia 5 katika Miezi Miwili ya mwanzo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 28, 2022
Faida za viwanda za China zaongezeka kwa asilimia 5 katika Miezi Miwili ya mwanzo
(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Takwimu za serikali Jumapili zilionesha kuwa, katika miezi miwili ya mwanzo ya mwaka 2022, faida za viwanda muhimu vya China zimeongezeka kwa asilimia 5 zikilinganishwa na kipindi hicho cha mwaka jana.

Idara ya Takwimu ya Taifa ya China (NBS) ilisema, kiwango cha ongezeko kimepanda juu kwa asilimia 0.8 tokea Desemba mwaka jana.

Thamani ya jumla ya faida za viwanda imefikia Yuan trilioni 1.16 katika miezi miwili hii, viwanda hivyo ambavyo mapato ya mwaka ya biashara ya bidhaa zao muhimu ni yasiyopungua Yuan milioni 20 (Dola za Marekani milioni 3.14)..

Mtakwimu mwandamizi wa NBS Zhu Hong alisema, kwa kukabiliwa na changamoto za kiuchumi za ndani na nje, sehemu nyingi na idara nyingi zimeongeza uungaji mkono kwa uchumi halisi, na hali hiyo ilihimiza ufufukaji wa viwanda wa hatua madhubuti katika miezi miwili ya Januari na Februari.

Ingawa faida zimeongezeka, Bw. Zhu anavitaka viwanda kutoongeza gharama, kwa sababu viwanda vya chini yao, hasa viwanda vidogo bado vinakabiliwa na shinikizo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha