

Lugha Nyingine
Reli ya TAZARA ni Njia ya Uhai wa Maisha ya Wazambia
(Picha inatoka China Daily.)
Kwa wafanyabiasha wa Zambia wanaopita mipaka kati ya nchi hiyo na Tanzania, treni za Mamlaka ya Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA) ni njia yenye nafuu zaidi kwa usafirishaji wa watu na bidhaa.
Reli ya TAZARA inayounganisha Dar es Salaam ya Tanzania na Kapiri Mposhi ya Zambia ilijengwa kwa msaada wa China katika miaka ya 1970. Katika wakati wa Kusini mwa Afrika kukabiliwa na msukosuko wa kisiasa, reli hiyo ililenga kuwa mlango muhimu wa kuelekea baharini kwa Zambia kusafirisha bidhaa nje.
Miongoni mwa watu wengi wanaoendelea kufaidika na huduma ya treni za TAZARA, Bw. Agnes Mumba mwenye umri wa miaka 42, ni mfanyabiashara wa kuvuka mipaka anayefanya kazi katika eneo la Kasama, mji mkuu wa Jimbo la Kaskazini la Zambia.
Mumba anafanya biashara ya vitu vya matumizi ya nyumbani na nguo, na amekuwa akiitumia treni za TAZARA kwa miaka 15 ya kufanya biashara ya kuvuka mipaka.
“Ninatumia treni ya TAZARA kila ninapokwenda Tanzania kununua bidhaa. Hii ni njia yenye nafuu kabisa kwa usafiri wangu, na inaniwezesha kupata faida kubwa zaidi,” alieleza.
Bw. Mumba alikuwa amesimama kwenye kituo cha treni cha TAZARA kilichoko Kasama, ambapo alikuwa akisubiri kupanda treni ya kwenda Nakonde, mji mdogo ulioko karibu na mpaka wa Zambia na Tanzania. Alisema treni za TAZARA zimesaidia kustawisha biashara ya Zambia.
Wakati watu wengi wanatumia treni za TAZARA kwa ajili ya biashara, wengine walisema, huduma za treni ni njia ya kipekee inayoaminika ya usafiri wao wa kutoka mji mmoja hadi mwingine, hasa katika sehemu ya kaskazini mwa nchi hiyo ambayo inasumbuliwa sana na hali mbaya ya mfumo wa barabara.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma