Marekani aliye mhusika kwenye msukosuko wa Ukraine:
Kueneza habari zisizo za kweli na kuzusha uvumi ili kuchochea migogoro na hali ya mambo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 30, 2022

 

Mchoraji wa picha ya katuni: Ma Hongliang

Tangu migogoro kati ya Russia na Ukraine itokee, baadhi ya vyombo vya habari na wanasiasa wa magharibi si kama tu hawajafanya kazi ya kuzishawishi Ukraine na Russia kufanya mazungumzo, bali wametoa nguvu ya kuzusha uongo mmoja baada ya mwingine.

Serikali ya Marekani na baadhi ya vyombo vya habari vinaendelea kunukuu“upelelezi” kwa kueneza habari zisizo za kweli na kuchochea hali ya mambo. Kabla ya kutokea kwa migogoro, kulikuwa na vyombo vya habari vya Marekani vilivyotoa habari zisizo za kweli; mara baada ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing kumalizika, baadhi ya vyombo vya habari vilinukuu “upelelezi” kwa kuzusha kuwa “upande wa China uliwahi kuitaka Russia ‘isivamie ’Ukraine wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing”; baadhi ya maofisa wa Marekani waliipaka China matope mara kwa mara, na kusema upande wa China “haina nia ya kushiriki kwenye aina yoyote ya suluhisho la kidiplomasia la suala la Ukraine”......

Marekani ikitaka kuipaka China matope, hakika inaweza kupata kisigizo kila mara. Katika suala la Ukraine, upande wa China wakati wote unafanya kazi ya kiujenzi ya kuzishawishi Russia na Ukraine zifanye mazungumzo. Lakini Marekani inaeneza habari zisizo za kweli bila kusita, na kutumia suala la Ukraine kuipaka China matope.

Kueneza uongo hakuwezi kuepusha wajibu wa upande wa Marekani, badala yake kunafichua kusudi lake la kweli la kutaka kupata faida yake kutokana na msukosuko. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha