Ufufukaji wa uchumi wa Marekani waendeleza ubaguzi wa kimfumo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 30, 2022

Watu wakitembea barabarani kwenye eneo la Times Square huko New York, Marekani, Februari 14, 2022. (Xinhua/Wang Ying)

NEW YORK – Kituo cha Maendeleo cha Marekani, ambacho ni taasisi huru na isiyoegemea upande wowote, Jumanne wiki hii kimetoa ripoti ikionesha kwamba, ufufukaji wa uchumi wa Marekani kwa sasa unafichua athari za kuendelea kwa ubaguzi wa rangi wa kimfumo, ubaguzi wa umri na uwezo katika soko la ajira.

"Hasa, watu wengi weusi -- haswa wazee na wenye ulemavu-- wanaendelea kupata pengo katika nafasi za ajira na kiuchumi," imesema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, uchumi ambao watu weusi mara kwa mara hukabiliwa na viwango vya juu zaidi vya ukosefu wa ajira kuliko watu weupe, hauwezi kuzingatiwa kuwa umefikia kiwango kamili cha ajira.

Kadhalika, kwa mujibu wa ripoti hiyo, ahueni ya kiuchumi ambayo hainufaishi kila mtu kwa usawa haitoi matarajio mazuri kwa ustawi wa muda mrefu wa uchumi na utulivu wa nchi hiyo.

"Janga la UVIKO-19 liliitumbukiza Marekani katika mdororo mkubwa wa uchumi ambao uliathiri wafanyakazi na familia kote nchini; hata hivyo, athari za mdororo huu wa uchumi pia zimefichua athari mbaya za ubaguzi wa kimfumo wa muda mrefu kwenye soko la ajira," kinabainisha kituo hicho katika ripoti yake.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha