Marekani aliye mhusika kwenye msukosuko wa Ukraine:
Kujaribu kushirikisha nchi nyingi kuiwekea Russia vikwazo, na kuzidisha hali ya mafarakano na mapambano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 01, 2022

Mchoraji wa picha ya katuni: Ma Hongliang

Tangu Februari 21 Rais Vladimir Putin wa Russia atangaze kuzitambua "Jamhuri ya Watu wa Donetsk" na "Jamhuri ya Watu wa Luhansk" ambazo ziko mashariki mwa Ukraine, nchi za Ulaya na Marekani zimeiwekea Russia vikwazo kwa pande zote.

Baada ya kutekeleza hatua mfululizo za vikwazo zikiwemo kufunga fedha za kampuni za Russia zilizowekwa katika nchi kadhaa za magharibi, kuweka vizuizi kwa kampuni ya Russia kutumia fedha muhimu za dola ya Marekani kufanya biashara ya kimataifa, nchi hizo za magharibi hata ziliwaweka paka na mbwa wa Russia kwenye orodha ya vikwazo.

Kabla ya hapo, Shirikisho la Kimataifa la Felidae lilitangaza rasmi vikwazo dhidi ya Russia, likitaka matawi yake katika nchi mbalimbali kuacha kuagiza paka wanaofugwa nchini Russia, na kupiga marufuku mashirika yenye uhusiano na Russia kushiriki katika maonesho na mashindano yanayoandaliwa na shirika hilo. Na mbwa wa Russia pia hawaruhusiwi kushiriki kwenye maonesho makubwa zaidi, yaani Maonesho ya Mbwa ya Crufts yaliyofanywa nchini Uingereza kuanzia Machi 10 hadi 13.

Kuweka vikwazo si hatua ya kimsingi yenye ufanisi wa kutatua matatizo wakati wote. Kutekeleza hatua ya kuweka vikwazo hakuwezi kuletea amani na usalama, na kutazidisha tu hali ya mafarakano na mapambano.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha