

Lugha Nyingine
Thamani ya jumla ya uzalishaji wa baharini yazidi yuan trilioni 9
(CRI Online) April 07, 2022
Picha iliyopigwa tarehe 25, Novemba, 2021 kutoka angani ikionesha malisho ya baharini yaliyoko Mji wa Qinzhou, Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua)
Taarifa ya takwimu za uchumi wa baharini wa China kwa mwaka 2021 iliyotolewa na Wizara ya Maliasili ya China inaonyesha kuwa, mwaka 2021, thamani ya jumla ya uzalishaji wa mazao ya baharini nchini China imezidi yuan trilioni 9 (sawa na dola za kimarekani bilioni 1.4), na kuchangia asilimia 8 katika ongezeko la uchumi la China.
Taarifa hiyo inaonyesha kuwa, uwezo wa utafiti na utengenezaji wa vifaa vya ngazi ya juu vya baharini umeongezeka zaidi, na baadhi ya teknolojia zenye uvumbuzi za uchumi wa baharini zimefikia kiwango cha juu cha kimataifa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma