Shanghai yajitahidi kuhakikisha ugavi wa mahitaji ya kila siku wakati maambukizi ya virusi vya korona

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 08, 2022

Tarehe 6, Aprili, 2022, wahudhumu wa afya wakichukua sampuli kutoka kwa wakazi ili kufanya upimaji wa virusi vya korona katika eneo la Putuo, Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua)

Shanghai inachukua hatua mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya kila siku ya wakazi wa huko, hasa mahitaji ya kimsingi ya wazee, akina mama na watoto, huku jiji hilo likiwa chini ya usimamizi wa muda mfupi wa kufungwa wakati maambukizi ya virusi vya korona yakiibuka upya.

Utoaji wa mchele, unga, mafuta na nyama ni wa kutosha mjini humo, na usambazaji wa kutosha wa mboga na nyama unaweza kuwasili Shanghai kutoka miji mingine wakati wowote, alisema Naibu Meya wa Shanghai Chen Tong kwenye mkutano na waandishi wa habari Alhamisi.

Chen alisema, maduka makubwa na masoko yamefungwa kwa muda kwa sababu ya maambukizi ya virusi vya korona ya hivi sasa. Uwezo wa utoaji na usambazaji wa vitu vya maduka kwenye tovuti pia umepungua kwa sababu ya hali mbaya ya maambukizi.

Shanghai itajitahidi kutatua matatizo ya ufanisi wa chini wa utoaji na upelekaji wa vitu ili kukidhi mahitaji ya kimsingi ya wakazi wa huko, alisema Chen.

“Kwa kupitia jumuiya za wakazi, mahitaji ya watu yatakusanywa, na watu wanaojitolea watapeleka mahitaji hayo kwa wakazi,” Chen alisema.

Shanghai inaanzisha orodha nyeupe ili kurejesha uendeshaji wa masoko, vituo vya utoaji na upelekaji, na maghala ya maduka ya mtandaoni yanayofuata kikamilifu hatua za kujikinga dhidi ya virusi vya Korona. Tatizo la ukosefu wa wahudumu wa kupeleka pia litatatuliwa kwa kuwaruhusu kurudi kazini wahudumu wa kutoka maeneo yasiyo na maambuziki ya virusi vya korona.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha