Rais wa IOC aandika barua kuwashukuru watu wa kujitolea kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 08, 2022

Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa Thomas Bach akihutubia sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 kwenye Uwanja wa Taifa wa Beijing, nchini China Februari 20, 2022. (Xinhua/Cao Can)

GENEVA – Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) Thomas Bach katika barua yake aliyotuma Alhamisi wiki hii ametoa shukrani zake na kuvutiwa na watu wote wa kujitolea waliohudumu wakati wa Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya baridi ya Beijing 2022.

"Ninapenda kutoa shukrani zetu za dhati na pongezi kwenu nyote, watu wa kujitolea wa Beijing 2022. Mnaweza kujivunia sana ukweli kwamba wakati Beijing ilipoweka historia ya kuwa mji wa kwanza duniani kuandaa aina zote mbili za Michezo ya Olimpiki ya majira ya joto na baridi, ulikuwa sehemu muhimu katika kuandika ukurasa huu mzuri katika historia ya Olimpiki," Rais wa IOC amesema.

"Mapenzi na shauku yenu ya kweli kwa Michezo ya Olimpiki ambayo nyinyi nyote mlionyesha ilikuwa ya kufurahisha sana. Wanamichezo tulihisi hivi, sisi sote katika jumuiya ya Olimpiki tulihisi hivi na tunawashukuru milele," ameendelea kuandika kwenye barua yake.

"Kwa niaba ya jumuiya nzima ya Olimpiki, nasema: asante, marafiki wa kujitolea, kwa mchango wenu mkubwa kwenye mafanikio makubwa ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi na Paralimpiki ya Beijing 2022. Tabasamu zenu zimechangamsha mioyo yetu."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha