Vyombo vya habari vya Ujerumani: Russia inalipa deni la nje kwa Ruble kwa mara ya kwanza badala ya dola za Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 08, 2022

Kwa mujibu wa habari ya Shirika la Habari la Deutsche mjini Moscow, Aprili 6, Russia ilitumia fedha zake za Ruble kwa mara ya kwanza kulipa deni lake la nje badala ya kutumia dola za Marekani, ambapo ililipa deni la Euro la dola za Marekani milioni 649.2.

Habari zilisema kuwa kwa sababu ya kuwekwa vikwazo vikali baada ya “kuivamia” Ukraine, benki moja ya Marekani ilikataa kuhamisha pesa kwa dola za Marekani, hivyo Wizara ya Fedha ya Russia ililipa deni lake kwa fedha zake za Ruble badala ya dola za Marekani.

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, ambaye pia ni Msemaji wa Rais wa Russia Dmitry Peskov alisema Tarehe 6 kuwa Russia haina sababu ya kutangaza kufilisika. Alisisitiza kuwa Russia ina rasilimali zote zinazohitaji kulipa madeni yake ya nje, pia alilalamika kuwa akiba “nyingi” za fedha za kigeni za Russia zimezuiliwa katika akaunti zake za benki za nje.

Kwa mujibu wa habari, Peskov alisema kuwa kama hali hiyo ikiendelea, Russia italazimika kulipa madeni yote kwa Ruble, na aliongeza kusema kuwa “kufilisika kwa Russia kwa sababu bandia” kutawezekana tu ikiwa malipo ya Ruble yatazuiliwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha