Marekani mwanzilishi wa mgogoro wa Ukraine

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2022

(Katuni na Ma Hongliang)

Mgogoro unaoendelea wa Ukraine ni matokeo ya mchezo wa siasa za kijiografia ambapo Marekani huitumia Ukraine kama chesi katika jaribio lake la kuishinikiza Russia katika mchakato wa hatua kwa hatua.

Kabla ya kuunganishwa tena kwa Ujerumani, Marekani iliahidi Umoja wa Kisovieti kwamba Muungano wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (NATO) hautapanua hata "inchi moja kuelekea mashariki." Hata hivyo, baada ya kumalizika kwa Vita Baridi, Marekani ilianzisha awamu tano za upanuzi wa NATO kuelekea mashariki, na kuzialika nchi 14 za Ulaya Mashariki na nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola Huru kujiunga na NATO, ikiendelea kupanua muungano huo kuelekea Russia.

Vikosi vya NATO vinavyoongozwa na Marekani viliishambulia kwa mabomu Belgrade bila kupata kibali cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuiangamiza Serbia na kuanzisha vita nchini Afghanistan, Iraq na Libya. “Yote haya yalichangia kuifanya Russia kuwa na hisia ya kuzungukwa”, anasema Msomi Andrei Makine wa Taasisi ya Ufaransa.

Marekani ilianzisha Mapinduzi ya Chungwa Mwaka 2004 na Mapinduzi ya Maidan Mwaka 2014 nchini Ukraine, iliunga mkono serikali ya Ukraine inayounga mkono Marekani, na kuishawishi Ukraine kujiunga na NATO, na kuifanya Ukraine kuwa kipande cha chesi katika makabiliano yake na Russia. Marekani, kwa kutumia nchi moja kama tegemeo lake kutishia kwa makusudi usalama na uvumilivu wa nchi kubwa, ndiyo mwanzilishi wa mgogoro wa Ukraine.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha