

Lugha Nyingine
Mji wa Guangzhou, China kusitisha kwa muda masomo ya ana kwa ana ili kudhibiti UVIKO-19
GUANGZHOU – Mji wa Guangzhou, ulioko Kusini mwa China jana Jumapili umetangaza kusimamishwa kwa muda kwa masomo ya ana kwa ana darasani katika shule za msingi na za sekondari kuanzia Aprili 11 ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona.
Ofisa kiongozi mmoja wa mji huo jana Jumapili amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba, kuanzia Saa 8 mchana Jumamosi hadi Saa 2 usiku jana Jumapili, mji huo ulikuwa umeripoti watu 22 walioambukizwa virusi vya Korona huku kukiwa na mlipuko mpya wa hivi karibuni wa virusi vya korona kuanzia Ijumaa ya wiki iliyopita.
Chen Xueming, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya mji huo amesema kwamba, kuanzia Aprili 11, wanafunzi katika shule za msingi na za sekondari za Guangzhou watatumia madarasa ya mtandaoni. Isipokuwa kwa wanafunzi wa darasa la tatu katika sekondari za juu ambazo shule zao zina malazi na hali ya usimamizi uliofungwa.
Shule za chekechea zitasitisha kwa muda kuwapokea watoto wapya. Taasisi za mafunzo ya nje zitasitisha mafunzo yake nje ya shule, na vituo vya kuwatunza watoto baada ya masomo shuleni vitasitisha huduma. Na vyuo vikuu vinatazamiwa kufanya usimamizi katika hali ya kufungwa .
Mtihani wa elimu ya michezo wa kujiunga na shule za sekondari za mji huo, ambao awali ulipangwa kufanyika Aprili 11, pia utasitishwa kwa muda.
Guangzhou pia imeimarisha hatua zake za kudhibiti virusi vya Korona na kuwahimiza wakaazi wake wasiondoke katika mji isipokuwa pale inapolazimu.
Chen Bin amesema, watu wamegunduliwa kuambukizwa virusi vya korona katika upimaji, hivyo huenda kuna mnyororo wa maambukizi kwenye maeneo ya makazi, hivi sasa maeneo kumi na moja ya Guangzhou yameanzisha kampeni jumuishi ya kupima virusi vya Korona. Kufikia jana Jumapili mchana, jumla ya watu zaidi ya milioni 19 walikuwa wamechukuliwa sampuli.
Kuanzia Jumapili alasiri, baadhi ya maeneo yamefanya upimaji wa wa umma, ambao unaaminika kuwa njia kuu ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Korona kwa wakati unaofaa.
“Hivi sasa, Guangzhou inajenga hospitali ya muda katika kituo chake cha maonyesho cha Pazhou” amesema Wu Linbo, Naibu Katibu Mkuu wa serikali ya mji wa Guangzhou.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma